Wednesday, 12 February 2020

MASAUNI ATOA AGIZO ALIPOZURU GEREZA KUU ARUSHA LEO

Na Ahmed Mahmoud,ARUSHA
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni  amesema gerereza Kuu La Arusha limeshindwa kufikia malengo ya kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya wafungwa katika mkoa huo.
Masauni amesema hayo jana Jijini Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika gereza hilo kwa ajili ya kufuatilia hali ya uzalishaji katika sekta ya kilimo haswa zao la maharage na mahindi.
Alisema serikali inalazimika kutumia kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua chakula cha kulisha wafungwa katika gereza hilo jambo ambalo siyo sahihi.
"Mnamiliki ekari 677 mnategemea kutumia kilimo cha hali ya hewa wakati mnaweza kutumia kilimo cha umwagiliaji nalitaka shirika la magereza kutoa fedha ili muanze kilimo cha umwagiliaji kuongeza tija ya uzalishaji haikunaliki chakula hakitoshi kulisha wafungwa huu ni uzembe"
Alisema ni hasara kwa serikali kuendelea kununua chakula wakati kuna nguvu kazi kubwa ya wafungwa ambao wamengweza kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha kulisha gareza hilo na magereza ya mikoa mingine.
Kwa mujibu wa Masauni magereza hiyo imeshindwa kitekeleza agizo la rais John Magufuli la kuzitaka magareza zote nchini kulima kilimo chenye tija ili waweze kujitegemea kwa chakula badala ya serikali kununua chakula cha wafungwa.
Kutokana na kilimo hicho kusua sua Masauni alilazimika kuwasiliana na Kamshina wa magereza nchini na kumtaka kuleta kiasi cha shilingi milioni  326 kwa ajili ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.
Alisema ni aibu kwa magereza hiyo kukosa kiasi hicho vha fedha licha ya kuwa na shamba kubwa pamoja na miradi mingine ikiwemo ya ufugaji na kutaka kiasi hicho cha fedha kitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vonhinevyo.
Kwa upande wake mkuu wa gereza  kuu la ArushaAndrew Mtamamiro  alikiri ni kweli wameshindwa kufikia malengo ya uzalishaji wa chakula kwa ajili ya wafungwa na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote ya Naibu waziri Masauni.

No comments:

Post a comment