Wazalishaji na Wafanyabiashara wa Bidhaa za Mbogamboga na Matunda pamoja na taasisi za kimkakati zinazosaidia katika mnyororo wa thamani wa mazao hayo ikiwemo TanTrade, TAHA & ITC wameshiriki kwenye Maonesho ya Fruit Logistica yanayofanyika katika nchi ya Ujerumani.

 Zaidi ya Kampuni 6 kutoka Tanzania zimefuzu ili kushiriki Maonesho hayo ambao wanauwezo wa kuuza bidhaa za Matunda na Mbogamboga nje ya nchi kwa viwango vinavyohitajika na Uwezo wa Uzalishaji. Maonesho haya yalianza tarehe 5 hadi 7 Februari, 2020. Katika Picha ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt Abdallah Possi akiwa na washiriki kutoka Tanzania.




Share To:

msumbanews

Post A Comment: