Sunday, 23 February 2020

BREAKING NEWS :WATUMIAJI WOTE WA VODACOM TANZANIA


Huduma ya Intaneti ya Vodacom imekuwa na hitilafu tangu asubuhi ya jumapili tarehe 23 februari 2020. Hii ni kutokana na kukatika kwa mkonga wa faiba ulioko baharini, upande wa Msumbiji ambao umechukua muda kurekebishika kutokana na mvua kali kwenye bahari ya Hindi.
Tumepata suluhisho la muda mfupi kutoka Seacom ambao ni washirika wetu wakuu watatupatia msaada kuhakikisha tunarejesha huduma hii kwa haraka iwezekanavyo.
Tunasikitika kwa usumbufu uliojitokeza kwa wateja wetu na tungependa kutoa shukrani za dhati kwa uvumilivu wenu na kwamba tunaahidi kutoa huduma ya Intaneti ya bure kwa wateja wetu pale huduma zetu zitakaporejea .
Asante.
Imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kampuni Vodacom, Rosalynn Mworia.

No comments:

Post a comment