Picha ya maktaba

Imeelezwa kuwa jamii wilayani Kahama mkoani Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya elimu ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kutokana na walio na ugonjwa huo kukimbilia kwa waganga wa kienyeji wakidai wamerogwa.

Hayo yamesemwa na mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na Ukimwi halmashauri ya mji wa Kahama Nkoba Luzumbi  alipokuwa akizungumza na  Mtandao huu ofisini kwake.


Amesema hali hiyo inasababishwa na jamii kukosa elimu ya kifua kikuu ambapo kwa mwaka 2020 wamejipanga kuwatumia wadau mbalimbali kuhakikisha elimu inawafikia wananchi ili kutokomeza ugonjwa huo ambapo takwimu za mwaka 2019 halmashauri ya mji wa Kahama imepokea wagonjwa 1,042 wakiwemo sita walio na kifua kikuu sugu.


Luzumbi amesema kundi jingine ambalo linachangamoto ya kushindwa kutumia dawa ya kifua kikuu ipasavyo ni wachimbaji wadogo  wa madini kwani wamekuwa wakihama migodi kila kukicha hivyo kwa mwaka huu vile vile wameandaa mpango mkakati wa kuhakikisha wanawasiliana na viongozi wa migodi ili kuendelea kuwahamasisha kutumia dawa.


Aidha halmashauri ya mji wa Kahama kwa mwaka 2019 imevuka lengo iliyopangiwa na wizara ya afya katika kuibua wagonjwa wa kifua kikuu ambapo walipan giwa kuibua wagonjwa 1001 lakini wamefanikiwa kuibua wagonjwa 1042 sawa na asilimia 104.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: