Thursday, 30 January 2020

TMDA YAFANYA UKAGUZI VIWANDA YA DAWA VINAVYOJENGWA DAR NA PWANI


NA MWANDISHI WETU.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), imefanya ziara ya kutembelea na ukaguzi wa viwanda 8 vya dawa za binadamu na mifugo vinavyoendelea kujengwa katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo aliambatana na wakaguzi wa viwanda kuangalia hatua zilizofikiwa katika ujenzi na kuendelea kutoa ushauri wa kitaalam ili kuwezesha viwanda hivyo kukidhi matakwa ya kisheria katika utengenezaji sahihi wa dawa  (GMP).

Ziara hiyo ya siku tatu iliyoanza Januari 27-29 mwaka huu, ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano.

Viwanda vilivyotembelewa ni:-
Vista Pharmaceuticals Ltd na Kariuki Pharmaceuticals vilivyopo Zegereni, Kibaha, Hester Biosciences Africa Ltd na Biotec Pharmaceuticals vya mifugo vilivyopo Kibaha, Emedics Pharmaceuticals kilichopo Kerege Bagamoyo.

Pia  Cure Pharmaceuticals Ltd kilichopo Kimbiji, Kigamboni, African Pharmaceuticals kilichopo Kisemvule Mkuranga na Alpha Pharmaceuticals Ltd kilichopo Mbangala Rangi tatu, Temeke.

Mwisho

No comments:

Post a comment