Friday, 3 January 2020

POLISI IRINGA YAWAKAMATA WACHINA KWA TUHUMA ZA KUTOROKA NA MADINI


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire
...........

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linawashikilia raia  wawili   wa  China   kwa  kutuhumiwa  kutapeli  madini wachimbaji  wadogo  wa wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe madini yao  na  kutoroka  nayo .

Kaimu  kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa  ACP Rienada Milanzi  alimweleza   mwandishi  wa habari hizi jana  kuwa  watuhumiwa  hao  Lin Fangquo (55) na Wei Sical (34)  walikamatwa majira ya saa 6.30 mchana katika  eneo la Mazombe Mji wa Ilula   wilaya ya  Kilolo  katika barabara  kuu ya Iringa – Dar es Salaam  disemba 31  mwaka jana wakijaribu  kutoroka . 

Milanzi  alisema  kuwa kukamatwa  kwa  raia  hao wa China  kulikuja  baada ya  kuwepo kwa taarifa  za  kipolisi  zilizokuwa  zikiwatafuta   watuhumiwa  hao  ambao  walikuwa  wanatafutwa na  jeshi la  polisi  mkoa wa Njombe  kwa  tuhuma za  kuwatapeli  wachimbaji wadogo madini yao bila  kuwalipa .

“ Jarada  la  kesi ya  watuhumiwa hao  lipo wilaya ya  Ludewa  mkoa  wa  Njombe  ambapo  walikuwa  wakitafutwa kwa jarada  namba LDW/IR/548/2019   jeshi la  polisi  limefanya  kuwakamata  kutokana na RB hiyo  ila  undani  wa   tuhuma  zao  upo mkoani Njombe “  alisema

Kuwa  watuhumiwa hao  walikamatwa  wakiwa na viroba  vitatu vyenye mawe  yenye uzito mbali  mbali  mifuko  mitatu mmoja ukiwa na  Kilo 43.40  za  mawe  yanayodhaniwa ni madini ya  kopa na mfuko  wenye   kilo 7.25  na mfuko wa tatu ulikuwa na kilo 9.5  ilikuwa na mawe yanayodhaniwa  kuwa na madini ya makaa ya mawe . 

Alisema  kuwa  sambuli  za mawe hayo zimepelekwa kwa  wataalamu  wa madini   ili  kuchunguzwa  Zaidi kabla ya  kusafirishwa  kwenda  mkoani Njombe kwa  ajili ya kufikishwa mahakamani  kwa  tuhuma  zinazowakabili .

Kamanda wa  polisi wa mkoa wa Njombe Hamisi Issa  alipopigiwa  simu na mwandishi wa habari hizi  ili kujua undani wa tukio  hilo na thamani ya madini ambayo  wachimbaji  wadogo  Ludewa  walidai  kutapeliwa alisema  kuwa bado  wapo  kwenye  uchunguzi Zaidi ili  kujua suala  hilo kwa  kina kamanda  huyo  alisema  wachina  hao wamekuwa  wakijishughulisha na ujenzi  wa barabara.


No comments:

Post a comment