Monday, 20 January 2020

MBUNGE WA ARUMERU ATOA MSAADA WA VYEREHANI 20 
Na Imma Masimba ,Mbuguni 

Mbunge wa Arumeru Mashariki  Dr.John Pallangyo ametoa msaada wa vyerehani 20 kwa wahitimu wa chuo cha Ufundi cha Next life kilichopo kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru ili kuwawesha wahitimu hao kujiajiri baada ya kumaliza masomo ili kujipatia kipato na kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza katika mahafali ya chuo hicho ,Mbunge huyo amesema kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo hawapaswi kukaa mitaani kusubiri kuajiriwa bali wanapaswa kuwa na uthubutu wa kujiajiri hivyo vyerehani hivyo vitawawezesha kujiajiri.

Dr.John amesema kuwa  ataendelea kuwaunga mkono vijana wenye nia ya kujikwamua kiuchumi  na kuchangia katika kufikia katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda kama ilivyo adhma ya serikali ya awamu ya tano.

Aidha amewataka vijana kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia nidhamu na uadilifu ili waweze kutimiza malengo yao na kufanikisha ndoto zao.

Anaeleza kuwa ataendelea kushirikiana na vijana  katika Wilaya hiyo katika masuala ya kimaendeleo pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kufanikiwa na kuchangia maendeleo katika familia,jamii na taifa.

No comments:

Post a Comment