Tuesday, 21 January 2020

MBUNGE MAVUNDE ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA ZUZU


Mbunge wa Dodoma mjini Anthon Mavunde akitoa msaada wa chakula kwa Mahanga wa mvua 
Mbunge Mavunde akizungumza na wananchi wake 
Sehemu ya chakula cha msaada 

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo amekagua miundombinu ya barabara na nyumba zilizobomoka katika kata ya Zuzu kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dodoma na kujionea mwenyewe uharibifu mkubwa uliojitokeza.

Pamoja na kukagua pia ametoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua hizo .

Akitoa taarifa,Diwani wa kata ya Zuzu Abdallah Awadh  amebainisha kwamba nyumba za jumla ya wananchi 286 zimepata uharibifu  hali ambayo imepelekea wengi kukosa makazi ya kudumu na kupoteza mali nyingi pamoja na vyakula huku miundombinu ya barabara ikiwa imeharibiwa kwa kiwango kikubwa.

"Nimekuja kukagua miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua na pia kuwapa pole wananchi ambao nyumba zenu zimebomolewa na mvua hizi,niwaombe wananchi tuendelee kuchukua tahadhari kutokana na mvua hizi ili zisilete madhara zaidi.Nitaendelea kuwa pamoja nanyi kutatua changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hichi na leo nimewaletea  unga wa sembe tani 1 magunia ya maharage na maji"
Alisema Mavunde

Wakitoa shukrani zao,Wananchi wa kata ya Zuzu wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna alivyojitoa katika matatizo ya wananchi na kuwajali katika shida zao kwa kuwapatia msaada ambao utawaondolea changamoto za chakula kwa wakati huu.

No comments:

Post a comment