Katika hali inayoonyesha ni ukatili wa kutisha watu  wanne wa familia moja ya mganga wa kienyeji  Petro Sagalika akiwemo mama mjamzito wameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na wananchi pamoja na kuchomewa vitu vya ndani na nyumba kubomolewa kwa kutuhumiwa kuwa ni wachawi .mwandishi wetu anaripoti toka Kasuru kigoma 

Tukio hilo limetokea   katika mtaa wa Katandala kata ya Msambara Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma ambapo awali marehemu walikuwa walituhumiwa kuhusika na vitendo vya ushirikina.

Waliouawa katika tukio hilo ni mzee Petro Sagalika ambaye alikuwa mganga wa kienyeji , mkewe Suzana Mkuka, na watoto wao Fonsi Petro na Aniza Petro aliyekuwa mjamzito.

Mtoto mkubwa wa marehemu Daud Sagalika amesema tukio hilo limeacha simanzi katika familia yao kutokana na wazazi na ndugu zao kuuawa kinyama na wananchi kwasababu ya imani za kishirikina.

Amesema wananchi hao wamefanya ukatili mkubwa ambao serikali inatakiwa kuchukua hatua ya kulinda usalama wao na kwa kuwa hawana hakika ya kuishi pamoja na kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.

"Wananchi wamewafanyia kitendo cha ukatili wazazi wangu na ndugu zangu kwa kuwauwa kinyama wamechukua sheria mkononi,tunaiomba serikali itulinde kwani hata sisi hatuna uhakika na usalama wetu pia watuhumiwa wote wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya dola"alisema

Ndugu mwingine wa familia hiyo Daud Sagalika amesema  tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia ijumaa ambapo kuanzia saa mbili usiku wananchi walianza kujikusanya na kuvamia nyumbani kwa baba yake na kuanza kuwashambulia kwa kuwachukua na kuwakatakata mapanga.

Alisema pamoja na kufanya mauaji hayo wamebomoa nyumba tatu za familia na kufyeka migomba na kwamba baada ya mauaji hayo polisi walichukua miili na kuifanyia uchunguzi na baadae kuruhusu familia izike ambapo miili hiyo imezikwa katika kati ya nyumba za familia hiyo.

Diwani wa kata ya Msambara Evansi Buchonko  alisema sababu kubwa ya mauaji hayo inatajwa kuwa ni imani za kishirikina ambapo marehemu mzee Saganila ambaye alikuwa mganga wa kienyeji alikuwa akituhumiwa na wananchi wa mtaa huo na vijiji jirani kuhusika katika mauaji ya baadhi ya watu.

Alisema walilazimika kuitarifu polisi usiku wa tukio ambapo polisi walifika na kukuta mauaji yalishafanyika ambapo marehemu wote walitolewa nje na kuuliwa barabarani nje ya nyumba yao huku baadhi ya wanafamilia wakifanikiwa kuokoka katika tukio hilo ambapo inasadikiwa pia baadhi ya watoto walijificha mashambani.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Pia ametoa onyo kwa wananchi ambao wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na kuwaua watuhumiwa na kwamba kufanya matukio kama hayo kwa imani za kishirikina ni kosa
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: