Mwanahabari wetu akizungumza na Erick Msuha 
  ERICK  Msuha  (47) mkazi wa Kijiji cha Narwanda kata ya Maguu Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambaye  anayesumbuliwa  na maradhi na kumsababishia kunywa maji lita 100 kwa siku  ili kuendelea kuishi ,amewaomba watanzania wamsaidie ili akatibiwe maradhi hayo .mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvuma

 Msuha akizungumza na mtandao huu wa Msumbanews  Nyumbani kwake Kijijini hapo alisema kuwa maradhi hayo yalimkuta baada ya kupigwa na radi mwaka 1993 na kumfanya aendelee kutaabika hadi sasa.

  Amesema kuwa baada ya kupigwa na radi alizimia kwa kupoteza fahamu kwa muda mrefu na alipopata fahamu akiwa katika Hospital ya misheni ya Litembo alijikuta kama anaendelea vizuri gafla hali ilimbadilikia na kuanza kunywa maji lita 80 kwa siku na sasa anafikisha lita 100.

 Amefafanua kuwa tangu mwaka 1995 hali ilivyombadilikia alienda Hospital mbalimbali hapa Nchini huku baadae watalaamu wa Hospital ya Rufaa ya misheni Peramiho waligundua kuwa kuna mifumo ya viungo kwenye mwili wake vimeharibika ikiwemo utumbo wa chakula na Koromeo limetoboka.

 Msuha amesema kuwa kwamujibu wa madaktari wa Peramiho walimuambia ili kufanikisha kurudi kwenye hali yake ya kawaida anatakiwa afanyiwe upasuaji ambao utakaogarimu Sh.Milioni 2.7 ambazo ameshindwa kuzipata na kuamua kuwaomba watanzania wenye mapenzi mema wamusaidie.

“Ninapata mateso makali sana mali zote nimeuza kwaajili ya kujiuguza ,mke wangu niliyefunga naye ndoa Gerumana Ndunguru ,amenitoroka mzigo mkubwa umebakia kwa baba yangu mzazi Januari Msuha pamoja na mwanangu Porotas Msuha ambao wanahangaika kunichotea maji ya kunywa lita 100 kila siku”amesema  Erick Msuha.

 Kwa upande wake mtoto Porotas (25)Msuha alisema kuwa hakuna siku aliyowahi kulala usingizi zaidi ya kukesha tu kwa kumpatia maji ya kunywa ambayo yanamfanya aweze kutapika na kuondoa gesi inayokuwa ipo tumboni .

“Ninashindwa hata kwenda kufanya vibarua ili kukidhi mahitaji ya Nyumbani hapa ,hivyo nawaomba watanzani wamsaidie baba yangu kwa kumpa mchango ambao utakao muwezesha kumpeleka akatibiwe”amesema Porotasi Msuha.

 Baba mzazi  Januari Msuha (72)amesema kuwa mwanaye Erick Msuha ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto nane ambao baadhi yao hawajulikani waliko kiasi cha kushindwa kumjulia hali ndugu yao jambo ambalo lisema linamuumiza  sana .

 Aidha kufuatia hali hiyo Erick Msuha aliyaweka mawasiliano yake wazi kama kuna mtu anahitaji kumsaidia awasiliane kwa No.0757-240221 na N0.0675-473105.

               
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: