Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiteta na mwakilishi wa CCM mkoa wa Iringa katika kikao cha bodi ya barabara mara baada ya kikao kumalizika
wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Suzana Mgonakulima (Chadema ) na Zainabu Mwamwindi wakiwa kwenye kikao
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kulia akiwa na mstahiki meya Iringa Alex Kimbe na mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Stephen Mhapa wakati wa kikao cha bodi ya barabara
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah na Mbunge wa Mufindi Kusini wakiwa katika kikao
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imepania kuuboresha uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa ili kuwezesha ndege kubwa kama bombardier na airbus zianze kutua katika uwanja huo mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa
Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa kikao cha bodi ya barabara mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa mkuu huyo wa mkoa alisema serikali imeendelea na uboreshaji wa uwanja huo na ipo mbioni kuuboresha zaidi ili kuwezesha ndege nyenye ukubwa wowote na hata ndege za mizigo kuutumia uwanja huo kutua na kuruka na mazao ya wakulima wa mkoa wa Iringa kama Parachichi na mengine .
Alisema kuwa serikali ya waamu ya tano ndani ya mkoa wa Iringa imeanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundo mbinu ikiwemo barabara ya Mafinga kwenda Kibao Mufindi kwa kiwango cha lami ,barabara ya Iringa - Hifadhi ya Ruaha na kuboresha uwanja wa ndege wa Nduli .
" Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli ameamua kutufanyia mambo makubwa zaidi mkoa wa Iringa pamoja na ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo ya uwekezaji wa viwanda na hifadhi yetu ya Taifa ya Ruaha ameamua kutenga fedha kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa Nduli ili kuweza kuwa na ubora wa kimataifa utakaowezesha ndege kubwa zote kutua katika uwanja huo " alisema Hapi
Alisema kuwa tayari taratibu za manunuzi katika upanuzi wa ujenzi wa uwanja huo zimeanza na kuwa tayari mfumo wa viwanja vya ndege wa kuweza kuongoza ndege kubwa kama aibus kutumia uwanja huo kutua na kuruka bila tatizo lolote .
Akizungumzia kuhusu hali halisi ya miundo mbinu ya barabara mkoa wa Iringa alisema mkoa una mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya Kilometa 5,810.30 ambapo wakala wa barabara nchini ( TANROADS ) unasimamia kilometa 1,212.36 na wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) unasimamia kilometa 4,597.94
Alisema upande wa barabara zinazosimamiwa na TANROADS kilometa 426.5 ni lami sawa na asilimia 35.1 ya barabara za TANROADS na kilometa 786.87 ni changarawe sawa na asilimia 64.9 ya barabara zote za TANROADS wakati kwa upande wa TARURA kilometa 97.30 ni lami sawa na asilimia 2.11 ya barabara zake na kilometa 1,318.62 ni changarawe sawa na asilimia 28.67 ya barabara zote na Kilometa 3,182.02 ni udongo sawa na asilimia 69.2 ya barabara za TARURA .
Hapi alisema kuwa katika kuhakikisha mkoa unakuwa na barabara zinazopitika muda wote serikali inayoongozwa na Rais Dkt Magufuli imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya matengenezo mbali mbali ya barabara ili kuhakikisha zinapitika muda wote ikiwemo wakati wa mvua nyingi .
Alisema kwa mwaka wa fedha 2018/2019 serikali ilitoa jumla ya shilingi 20,138,711,144.79 ambapo kiasi cha shilingi 14,346,000 zilitolewa kwa TANROADS na na shilingi 5,779,365,144.79 zilitolewa kwa TARURA kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa barabara katika mkoa wa Iringa .
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutowatoza wananchi gharama ya greda la Manispaa kwa ajili ya kutengeneza barabara za mitaa kwani kazi hiyo inapaswa kufanywa na Manispaa sio wananchi .
MWISHO
Post A Comment: