Saturday, 28 December 2019

UVCCM MKOA WA PWANI WAPATA MWENYE KITI MPYA


Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Pwani leo hii umefanya Uchaguzi wa kumpata mwenye kiti wake mpya baada ya aliyekuwa hapo awali kuteuliwa kuwa Katibu tawala wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es salaam,

Alikuwa ni SAMAHA SEIF SAID kutoka wilaya ya Mafia ndiye aliyeibuka kidedea wa nafasi hiyo dhidi ya MARRY DANIEL kutoka wilaya ya kibaha mjini,

Mkurugenzi wa Uchaguzi huo alimtangaza ndugu SAMAHA SEIF SAID Kwa kupata Kura 208 dhidi ya Kura 137 za MARRY DANIEL huku Kura zilizoharibika zikiwa 4 pekee,

Vijana hao wa Uvccm kutoka katika wilaya zote mkoa wa Pwani wameahidi kushirikiana Kwa nguvu zote na bi SAMAHA S SAID kwaajili ya kuliendeleza gurudumu la vijana kwaajili ya maslahi mapana ya Chama cha mapinduzi,

Naye bi SAMAHA S SAID mbali na kuwashukuru wajumbe wote waliojitokeza kumwamini na kumchagua ameahidi kuitendea haki nafasi hiyo na kuwahakikishia kuwa Yuko imara kweli kweli,

Mbali na Hilo aliyekuwa mwenye kiti uvccm mkoa wa Pwani bi Charangwa selemani makwiro alifika ukumbini hapo kwaajili ya kukabidi nafasi hiyo Kwa aliyechaguliwa Bi SAMAHA S SAID huku wajumbe waliojitokeza wakionyesha furaha zaidi na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko Ilala.
#msumbanewsapdates

No comments:

Post a comment