Baadhi ya walipa Kodi wa  Dar es salaam wanaendelea kupata kero katika jengo la Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) samora,

Walipa Kodi hao licha ya kuhamasika kulipa Kodi vizuri toka serikali ya awamu hii ya tano ilipoingia lakini wamelalamikia kitendo cha kuwekewa masharti magumu na mamlaka hiyo katika harakati za kubalisha majina kwenye kadi za magari , kupatiwa kadi nyingine pale ya zamani ikipotea.

Baadhi ya wateja wakizungumzia  changamoto hiyo  ambayo wanakutana nayo wateja hao huku pia wakizidi kutapeliwa na baadhi ya vishoka kwa ajili ya kurahisishiwa kazi zao huku watumishi wa mamlaka hiyo wakiwa wakali kwenye kusikiliza shida zao,

Kero kubwa ambayo  walipa Kodi wamezidi kuilalamikia ni pamoja na Sheria inayomtaka mmiliki wa chombo cha moto kutaka kubadilisha jina la Kadi ,au kama kadi ya gari imeungua Moto ni pamoja na kuwa na tangazo la gazeti linalomtaka awenalo ndani ya mwezi mmoja na wakati viambatanisho vingine vya ripoti ya polisi akiwa navyo hasaidiwi, hivyo ni lazima awe  na tangazo hilo ambao Kwa wananchi  wengi wao wameendelea kukimbia kituo hicho na kwenda mikoani ambako inaonyesha hakuna masharti magumu kama hapo samora,

Wakizungumza Kwa nyakati tofauti wananchi hao wameiomba serikali kupitia wizara ya fedha kuwasaidia na kuondoa vikwazo vingi wanavyokutana navyo ili waendelee kupata huduma Kwa wakati na haraka,

"Hivi sasa kumekuwa na usumbufu mkubwa Sana kama unavyoona hapa samora yaani watumishi hawajiongezi kurahisisha huduma, serikali inataka kukusanya Kodi lakini Baadhi ya watumishi wamekuwa wakituwekea masharti magumu Sana na kupelekea vishoka kutudhulumu pesa ,hii si Sawa hata kidogo,

Kwa mfano mm nina viambatanisho vyote vya ushahidi lakini wananiambia mpaka niende kwenye magazeti sasa naenda kumtangazia Nani wakati vyeti na Kadi zilizoungua ni vyangu na nipo tayari kulipa gharama zote ili nirudishe vitu vyangu, Tunaomba wahusika waliangalie hili, hapa tunalipa sh 50,000 kwaajili ya kutolewa Kadi iliyopotea, lakini kuna gharama kubwa nje ya Tra wanayotaka tuende kwenye magazeti kwanini?-


Hata baada ya kufuatwa msimamizi  msaidizi wa eneo Hilo la Samora Tra lililopo Dar es salaam kuulizwa aoijibu kuwa hawezi kwenda kinyume na maagizo na taratibu ni lazima wananchi watangaze kwenye magazeti na waje na vipande hivyo vya gazeti Kwa uthibitisho.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: