Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na wananchi waliojitokeza katika stendi ya hiace Kilombero Jijini Arusha,kulia kwake ni mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum,katika kampeni ya usajili wa laini za simu kwa mfumo wa vidole iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akimpa maelekezo Afisa wa NIDA Juliety Robert juu ya kuweka dawati kwaajili ya kuwasaidia wananchi ambao wanamalalamiko .
 Mkuu wa kandaya kaskazini TCRA Mhandis Imelda Salum (Mwenye tisheti nyeupe),kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro,wa kwanza kushoto ni Afisa NIDA mkoa wa Arusha Juliety Robert ,wa kwanza kushoto ni Katibu Tarafa wa Themi Felisian Gasper Mtahengelwa .
 Afisa wa NIDA mkoa wa Arusha akitoa ufafanuzi wa Jambo kwa mkuuu wa wilaya Gabriel Daqqaro,kushoto kwake ni mkuu wa kanda ya Kaskazini TCRA imelda Salum.
 Mkutano ukiendelea katika stendi ya hiace kilombero.
 Wananchi wakiwa katika viwanja vya Stendi ya Haice ya Kilombero wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Arusha.

Kutoka kushoto ni mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro katika stendi ya Hiace Kilombero
Afisa wa NIDA mkoa wa Arusha Juliety Robert akitoa ufafanuzi kwa wananchi mara baada ya kutoa malalamiko kwa.mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro kwamba wengine waneandikishwa zaidi ya mara tatu.




Mkuuu wa wilaya ya Arusha akisalimiana nawananchi katika tamasha la kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika stendi ya hiace kilombero Jijini Arusha jana.


Wananchi waliojitokeza kufuata namba zaonkatika stendi ya Hiace Kilombero Mkoani Arusha kwenue Kampeni ya Usajilinwa simu kwaalama za vidole iliyoandaliwa na TCRA kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akiwa amewasili katika stendi ya  Hiace Kilombero katika kampeni ya kusajili laininza simu kwa mfumo wa alama za vidoleniliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akisalimiana na wananchi waliojitokeza katika stendi ya Kilombero Jijini Arusha wengi wao wakiwa ni wafanya biashara .
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akijisajili kwa alama ya Vidole kwenye kampuni ya simu TTCL tayari katika viwanja vya Stendi ya haice Kilombero Jijini Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akijisajili kwa alama ya Vidole kwenye kampuni ya simu TTCL tayari katika viwanja vya Stendi ya hiace Kilombero Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya Kaskazini imewataka wananchi imewataka watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchukua tahadhari dhidhi ya utapeli kwenye mitandao ya simu za mkononi wala kutekeleza maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa maandishi hata kama yanatoka kwa namba ya mtu wanaomfahamu.

Akitolea ufafanuzi juu ya jambo hilo jana,  Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum katika tamasha la uhamasishaji wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole Jijini Arusha ,amesema Sheria inamtaka mtumiaji au anayenunua laini ya simu kuisajili majina halisi kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na posta (EPOCA) amewataka  taarifa wanazozitoa wakati wa kusajili laini za simu  ziwe za kweli kwani ni kosa la jinai kutoa taarifa ambazo siyo sahihi.

 ''Ikithibitishwa Mahakamani kuwa umetoa taarifa za uongo,adhabu kali hutolewa ikiwa ni pamoja na faini kifungo au vyote viwili,sajilini laini zenu za simu kwa usahihi kabla ya muda uliowekwa wa desemba 31 kumalizika''alisema

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ameiomba Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kuongeza  uhamasishaji wa watu kusajili laini za simu zao,  hadi siku za Jumapili, ili kufikia laini milioni 47
zilizolengwa kusajiliwa.

Daqqaro  alisema,hadi sasa laini zilizosajiliwa ni milioni 19 nchi nzima, idadi  ambayo ni ndogo ikilinganishwa na  idadi iliyotarajiwa  milioni 47 hivyo amewataka wananchi wa Jiji la Arusha ifikapo desemba 31 mwaka huu kila mmoja awe ameshasajili laini yake ya simu ya mkononi.

Kutokana na idadi ya waliojiandikisha kuwa ndogo, natoa  hamasa kwa

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuongeza juhudi na
kufanyakazi hadi siku ya Jumapili kuandikisha watu ili  kuwafikia
wananchi,”alisema.

Daqqaro alisema zoezi hilo la usajili linatambulika kisheria na kiutaratibu,hivyo uwepo wa usajili kwa njia ya alama za vidole gumba,
itasaidia kuwa na kanzi data yakujua takwimu za watumiaji wa mitandao
ya simu kila mikoa na  kupunguza wimbi  la utapeli na uhalifu wa
mitandao na kuimarisha usalama.

"Zoezi hili ni zoezi nyeti sana na mtu anapofanya usajili wa laini

yake analazimika  kutumia kidole chake, ili kupata taarifa muhimu  na
pale anapofanya uhalifu  atajulikana,  hivyo kwakiasi itapunguza
uhalifu,”alisema.

Aidha alisema katika uzinduzi huo ananchi wengi amejitokeza kusajili

laini zao, lakini changamoto inayojitokeza  baadhi ya wananchi
kutokuwa na vitambulisho vya Nida.

“Lakini sisi kama serikali naahidi tutaongeza  mashine  ili kuondoa

msongamani huu ninaouona wa wananchi  ilia pate huduma ka haraka na
kwenda kuendelea na shughuli za uzalishaji mali,”alisema.

Aliataka  makampuni ya  simu yanayotoa huduma katika viwanja hivyo vya

standi ya daladala kuhakikisha  yanasogeza huduma kwenye  maeneo ya
soko na mikusanyiko ya watu ili kuwafikia walio wengi.

Awali baadhi ya wananchi waliohudhuria kampeni hiyo, Huruma Juma na

Sophia Ismail waliomba NIDA kupunguza urasimu eneo la Kisongo na
kufanya kazi siku za Jumapili, ili kuondoa msongamano wa wananchi
anaojitokeza kusajili laini zao.

Kampeni hizo za usajili wa laini za simu zinaishia Desemba 31 mwaka

huu na  zinaratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  yenye
kauli mbiu  "Aachwi mtu nyuma, kamilisha usajili".


Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: