Wakati midajala  ikitawala juu ya Ndege kulamatwa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa  ndege aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imeshikiliwa nchini Canada  sasa imeachiwa .
Rais Dkt Magufuli ameyasema hayo leo Alhamisi wakati  akifungua semina ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho Taifa (NEC) iliyofanyika Jijini Mwanza.
“Taarifa tu ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa nchini Canada imeachiwa kwahiyo mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokelea hapa Mwanza,” amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo alisema wananchi watatangaziwa rasmi siku ya Ndege hiyo kuwasili nchini .

Hii ni mara ya pili kwa ndege ya nchi hiyo kuzuiliwa nchini Canada.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya Ndege hiyo kukamatwa alipata kuthibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni.
Kiwa sababu ya kukamatwa kwa ndege hiyo, kwa mujibu wa Prof Kabudi ni kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia Hermanus Steyn.
Steyn pia alifungua kesi nchini Afrika Kusini mwezi Agust iliyosababisha ndege aina ya Air Bus 220-300 izuiliwe na hatimaye serikali ya Tanzania kushinda kesi mahakamani
"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, ailisema mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: