Sunday, 22 December 2019

MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI TAIFA AZINOA ASASI RUVUMA


Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi  Taifa Jaji mstafu Meristela Longway katikati akizungumza na wadau wa Asasi mbalimbali za Kiraia zilizopo mkoani Ruvuma juu ya umuhimu wa kwenda kutoa elimu kwa jamii juu ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga Kura,ambalo zoezi lake litaanza Desemba 30 mwaka huu na kuishia Januari tano mwaka 2020.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kutoka asasi mbalimbali za Kiraia zilizopo mkoani Ruvuma  wakiwa kikao  hicho  MJUMBE wa tume ya uchaguzi Tanzania Jaji mstafu Maristela Longway amewataka Watanzania ambao wamefikia sifa za Kupiga Kura wametakiwa kujitokeza kwenye Vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga Kura ili nao waweze kupata fursa ya kupiga Kura katika uchaguzi wa mwaka 2020.Mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvum

Mjumbe huyo alitoa rai hii  wakati akizungumza na wadau wa kutoka katika asasi mbalimbali za Kiraia zilizopo  Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakati wa  mkutano wa elimu juu ya umuhimu wa Watanzania kujiandikisha kwenye daftari hilo ambalo litahifadhi taarifa za Mpiga Kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

  Longway  aliwataka viongozi wa vyama vya Siasa pamoja na  Viongozi wa  Dini amesema kuwa watu wenye sifa za kupiga kura wakijitokeza kwa wingi  kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zao katika daftari  la Kudumu la mpiga kura ili kutimiza wajibu wao wa kikatiba.

  Aidha amesema   asasi za kiraia ambazo zitakazo pewa vibali na tume zita takiwa zikafanye kazi hiyo ya kupita kutoa elimu ya mpiga Kura  kwa watu hao ili waweze  kujiandikisha kwenye daftari hilo ,ambalo zoezi hilo litaanza disemba 30 mwaka huu na kuishia januari tano mwakani .

 “Wadau wetu tunawaamini sana na ndiyo maana tumewaita ili tupeane uelewa kwa pamoja na hatimaye mwisho wa siku kila mtanzania mwenye sifa zilizoanishwa kwa mujibu wa sheria aweze  kutumia haki yake ya kupiga Kura “amesema mjumbe wa tume ya uchaguzi Meristela Longway.

 Kwa upande wake  mkaguzi wa Uhamiaji mkoani Ruvuma Ambinga Swai amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya watu wakutoka Nchi jirani zilizopakana na Tanzania hasa kwa mkoa wa Ruvuma wanatokea Msumbiji na Malawi kujipenyeza kinyemela na kujifanya nao ni wazawa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

 Swai amefafanua kuwa hata kama mtu kazaliwa Tanzania na kusoma hapo hakumpi fursa ya kujiita ni mzawa wakati wazazi wake walihamia kutoka nchi nyingine, hivyo jamii inatakiwa kuwatambua watu hao kisha kupeleka taarifa kwenye ofisi za uhamiaji.

 Naye mmoja wa wadau ambaye anatokea katika kundi la  baraza la machifu na manduna mkoani humo Agnellus Lugomi amesema kuwa mafunzo hayo walioyapata wataenda kuyatumia vema kwa kuielimisha jamii wenye sifa ya kuwa na vitambulisho vya Mpiga Kura waweze kujiandikisha kwenye daftari hilo.

                  

No comments:

Post a comment