Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus akimpa pole mmoja wa wananchi wake Leo, bonde la Msimbazi waliokumbwa na Mafuriko (katikati) meya wa Ilala Omary Kumbilamoto
Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus wa pili kushoto akimpa pole mmoja wa wananchi wake bonde la  Msimbazi waliokumbwa na mafuriko
 ....................................................
NA HERI SHAABAN
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli amewataka wananchi wa bonde la Msimbazi wasiendelee kukaa katika maeneo hatarishi .
Bonnah aliyasema hayo Leo wakati wa ziara yake ya kuangalia athari za mafuriko na kuwafariji wananchi walioathirika kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. 
Katika ziara hiyo Mbunge Bonnah aliongozana na Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto na Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala comrade Al Haji Said Sidde.
Akizungumza Mara baada ya kuona athari hizo Kamoli aliwaasa wananchi wanaoishi kando ya bonde hilo akisema kwa sasa wanatakiwa wapishe eneo hilo si salama kwa maisha yetu Mvua zinaendelea kunyesha na hazitupi taarifa!
Tunapaswa kufuata ushauri wa wataalam wetu wa hali ya hewa ambao wamesema kuwa wakati wowote mvua inaweza kunyesha
Hivyo nawashauri mpishe eneo hili mpaka mvua zitakapoacha kunyesha huku tukiisuburi serikali ijenge kingo za mto Msimbazi.
Mvua zilizonyesha juzi zimeleta athari maeneo mengi Katika wilaya ya Ilala na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla hususani Bonde la mto Msimbazi hasa jimboni la segerea wananchi wa kata za Kipawa, Kinyerezi, Vingunguti, Liwiti, Tabata, Kimanga na Buguruni wameathirika.
"Ziara hii ni endelevu na tumeianza jana ambapo tumezitembelea kata za Buguruni na Mnyamani na Leo Vingunguti " alisema Bonnah .
Naye Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amewapa pole familia zilizokumbwa na mafuriko haya na kuwataka wazingatie ushauri unaotolewa na viongozi hasa kuhusu kuondoka katika maeneo hayo ambayo si Salama.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: