Mlozi akifundisha kuishi wa lishe bora 
Washiriki wa kongamano la lishe mkoa wa Iringa wakifuatilia elimu 
Mlozi akifundisha utayarishaji wa mboga 
Katibu mkuu wa UWT Taifa Queen Mlozi  wa pili kushoto wakicheza na wenyeji wake 
Mkurugenzi wa TAHEA Lediana Mafulu Mng'ong'o  akitoa nasaha zake kwa mgeni rasmi 
Mkurugenzi wa TAHEA Lediana Mafulu Mng'ong'o  kulia akimpokea katibu mkuu wa UWT Taifa Queen Mlozi 
Katibu mkuu wa UWT Taifa Queen Mlozi  akisalimiana na viongozi wa dini 

.................................

Katibu mkuu wa jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania (UWT)Queen Mlozi ametambua na kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya  Tanzania Home Economics Association (TAHEA-IRINGA) Lediana Mafulu Mng'ong'o katika kupambana na lishe bora kwa watoto nchini .

Huku akikemea tabia zisizofaa za baadhi ya wanaume wanaoendekeza ulevi wa kupindukia na hata kunyonya maziwa ya mama anayenyonyesha haiku kwa imani ya kukata pombe kuwa si sawa maana hawawatendei haki watoto ambao wanastahili kunyonya maziwa hayo kwa lishe bora .

Kuwa TAHEA chini ya mkurugenzi wake Lediana ambae ni mmoja wa viongozi ndani ya UWT imekuwa ni chachu kubwa katika harakati za vitendo katika kutoa elimu kwa jamii juu ya lishe bora jambo ambalo ni la kupongezwa na kuigwa .

Katibu mkuu huyo alitoa pongezi hizo wakati wa kongamano la lishe mkoa wa Iringa lililofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Afya mjini Iringa pindi akifungua kongamano hilo .

Alisema kuwa suala mkurugenzi huyo amekuwa ni mfano mwema na ni msaada mkubwa kwa UWT si tu kwa mkoa wa Iringa bali kwa Taifa zima kutokana na harakati zake nzuri za kusimamia mambo ya msingi ambayo ni Ukombozi kwa mwanamke ,watoto na watanzania kwa ujumla juu ya lishe bora .

Mlozi alisema wakati TAHEA inaendeleza mapambano dhidi ya lishe bora bado kuna haja ya mkakati huo kuchukuliwa na mikoa yote kuona elimu bora ya lishe bora ambayo watoto wanapaswa kupewa inaendelea kutolewa ili kuliepusha Taifa na tatizo la udumavu na utapiamlo ambao umeikumba baadhi ya mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kama mkoa wa Iringa ,Njombe ,Mbeya na mikoa mingine jambo ambalo ni aibu kubwa.

"Kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya mwenyekiti wetu wa UWT Taifa mama Gaudensia Kabaka naomba nikupongeze sana mjumbe wetu wa baraza Taifa Lediana Mafulu  Mng'ong'o kwa kazi nzuri unayoifanya ndani ya mkoa wa Iringa maana hata inayofanywa ni mambo makubwa na mazuri ambayo tunataka na kuhitaji kwa maana sisi tuliposema tunawaita wewe ulikuwa umekwisha anza kwa sababu si kitu rahisi kufungua ofisi zinazozingumzia masuala ya lishe ndani ya mikoa 21 Tanzania sisi tunatambua kazi yako kubwa nawe ni hazina kubwa kwa Taifa " alisema katibu mkuu UWT Taifa 

Kuwa kazi za mkurugenzi huyo wa TAHEA zinaonyesha wazi kuwa zimelenga kumkomboa mwanamke ni ni dhahiri zinaonyesha jinsi ambavyo Mungu alivyoumba kuwa mwanamke ni kuwa msaidizi wa familia huku baba ni kichwa cha nyumba hivyo lishe bora kwa familia ni hitaji la Taifa .

Hata hivyo Mlozi alipongeza pia kazi zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na katibu tawala wa mkoa huo Happines Seneda katika harakati za kuunga mkono jitihada za lishe bora kwa mkoa wa Iringa na kuwaomba kuzidisha mapambano hayo .

Akizungumzia wanaume wananyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha ili kukata pombe alisema kuwa wanaume wenye tabia hizo wanapaswa kubadilika na kuwa tabia hiyo zaidi ameisikia mkoa wa Iringa japo anaamini ulevi upo mikoa yote hivyo ni vizuri wanaume kujitambua na kuacha tabia hiyo kwani ina mnyima lishe bora mtoto .

Awali wakizungumza katika kongamano hilo mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nicolina Lulandala  ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah na makamu mwenyekiti wa ALAT Taifa Stephen Mhapa walisema TAHEA imeonyesha njia ya kila makundi kufanya kazi ya elimu ya lishe sehemu yake .

Huku naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiahidi kufikisha elimu hiyo katika baraza la madiwani ili iwekewe mkazo na kutungiwa sheria ndogo itakayosimamia lishe bora ndani ya Halmashauri hiyo .

Kongamano hilo la aina yake lilishirikisha makundi mbali mbali ya jamii kama wanasiasa kwa maana ya viongozi ,wanahabari ,wasanii ,viongozi wa dini na makundi mengine .

Akizungumzia hali ya lishe ndani ya mkoa wa Iringa Mng'ong'o alisema kuwa hali ya lishe si nzuri na inapaswa elimu kutolewa zaidi .

Kuwa hali ya lishe ya watoto kwa Iringa ni asilimia 71,Mufindi 58,Kilolo 39  na hali ya ulishaji watoto Iringa ni asilimia 25,Mufindi 17na Kilolo 16 wakati kiwango cha matumizi ya pombe kwa wanawake wanaonyonyesha Iringa DC ni asilimia 28,Kilolo 30 ,na Mufindi 38.

Alisema madhara ya pombe ni pamoja na kupelekea kudharirika ,inapunguza hamu ya kula ,inaleta magonjwa ya ngozi ,inapelekea uvivu wa kupunguza umakini katika kazi inaongoza ajali na vifo vitokanavyo na ajali ,watoto wachanga kulaliwa hadi kufa na wazazi wao wakiwa wamelewa na inapelekea upunguvu wa chakula katika kaya .

Alisema TAHEA na CUAMM zinatekeleza mradi wa tabialishe katika mkoa wa Iringa na Njombe lengo likiwa ni kuchangia kupunguza udumavu wa watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 44 kwa mwaka 2013 hadi asilimia 35 ifikapo mwaka 2019.1
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: