Mwenyekiti mshindi ni Mwandishi Mkongwe Claud Gwandu aliyeibuka mshindi kwa kura 30 dhidi ya Sitta Tuma aliyepata kura 17.akizungumza na waandishi mara baada ya kupata ushindi huo.
Makamu Mwenyekiti  Ramadhan Libenanga akizungumza mara baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu wa JOWUTA uliofanyika Dodoma,wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa JOWUTA Suleiman Msuya akiyeshinda kwa kupata kura 44
 Maureen Odunga, Mwekahazina CHAMA cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania  (JOWUTA),

Said Mmanga amechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu kwa kupata kura 46 za ndio na mbili za hapana.
 Wa kwanza kushoto Veronica Ignatus ambaye alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa mdhanini wa JOWUTA,pamoja na Mussa Juma ambaye (hayupo pichani)

 Wa kwanza kushoto ni Saphia Ngalapi aliyechaguliwa na wajumbe wa  mkutano mkuu kuwa mdhamini wa chama.
Ndugu Sitta Tuma (aliyevaa miwani )akimpongeza Cloud Gwandu mara baada ya kutangazwa mshindi wa kuwa mwenyekiti wa JOWUTA Taifa

Wajumbe wa mkutano mkuu JOWUTA  wakiwa katika ukumbi Mkutano wa Maktaba kuu Mkoani Dodoma.
 Picha ya Pamoja ya waandishi pamoja na viongozi wa JOWUTA mara baada ya Mkutano mkuu kumalizika mkoani Dodoma.
Picha ya Pamoja ya waandishi pamoja na viongozi wa JOWUTA mara baada ya Mkutano mkuu kumalizika mkoani Dodoma.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

CHAMA cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania  (JOWUTA), kimepata viongozi wapya ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mkoani Dodoma ndipo ulipofanyika uchaguzi huo katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma ambao wanachama 48 walishiriki kati ya 61 waliothibitisha kushiriki wengine walishindwa kutokana na sababu mbalimbali.

Akitangaza washindi katika uchaguzi huo,Mwenyekiti wa Uchaguzi Keneth Ngelesi,alimtaja ndugu Cloud Gwandu mwandishi mkongwe kuwa ndiye aliyeibuka na ushindi wa kuwa mwenyekiti wa JOWUTA Taifa  kwa kura 30 dhidi ya Sitta Tuma aliyepata kura 17.


Ngelesi alitangaza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa na mgombea mmoja Ramadhan Libenanga ambaye alipata kura 43 za ndio na nne hapana.

Aidha chama hicho kinatambulika kisheria na kilipata usajiliwa mwezi Machi 2018 ,kwa sasa kina jumla ya wanachama zaidi 120 katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tabora, Arusha, Mbeya na Mwanza.

Aidha mshindi katika nafasi ya Katibu Mkuu wa JOWUTA mshindi ni Suleiman Msuya kwa kupata kura 44 za ndio tatu hapana na moja iliharibika na Said Mmanga amechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu kwa kupata kura 46 za ndio na mbili za hapana," alisema.

Mwenyekiti huyo alisema katika nafasi ya mweka hazina wajumbe walimpigia kura 47 za ndio Maurine Odunga kuendelea kushika nafasi hiyo huku kura moja ikiwa ya hapana.

Wengine waliochaguliwa na  wajumbe wa mkutano mkuu ni pamoja na  Veronica Ignatus, Mussa Juma na Saphia Ngalapi kuwa wadhamaini wa chama hicho kwa muda wa miaka mitatu kama katiba inavyoonyesha.

Mwenyekiti mpya wa JOWUTA, Gwandu akizungumza baada ya uchaguzi huo alisema kuwa mafanikio ya chama hicho yatatokana na wanahabari wenyewe kukijenga.

Gwandu aliwaomba waandishi wote nchini kutumia chombo hicho kupigania haki, maslahi  na maendeleo yao na nchi.

''Nawaomba wenzangu tushitikiane kuijenga JOWUTA na ili hilo lifanikiwe ni wajibu wa kila mmoja kutafuta wanachama kuanzia 10 wajiunge tuende pamoja kudai haki zetu kisheria," alisema Gwandu.


Mwenyekiti hiyo aliwataka wanachama wajitahidi kulipa ada ya kila mwezi ili kuwezesha chama kujiendesha chenyewe na kufuatilia stahiki za waandishi kisheria.

Mbali na uchaguzi wa viongozi mkutano huo ulifanya mabadiliko ya kiingilio kutoka shilingi 5,000 na kuwa shilingi 10,000/.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya Jowuta kuwa chini ya uongozi wa muda ambapo Said Mmanga alikuwa Mwenyekiti, Saphia Ngalapi, Makamu Mwenyekiti, Samson Kamalamo, Naibu Katibu Mkuu na Maureen Odunga, Mwekahazina.

Jowuta ilisajiliwa Machi, 2018 baada ya Mahakama Kuu, kitengo cha Kazi kukifuta kilichokuwa Chama cha Wafanyakazi Waandishi wa Habari Tanzania (TUJ), mwaka 2014, kufuatia maombi ya msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri.

Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: