Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Murroto ametolea  ufafanuzi juu ya kifo cha ustadhi Rashid Ally Mussa (62) ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya The Dalai Islamic Center na Mmiliki wa shule ya ZAMZAM Mkazi wa Chang’ombe Extension kuwa alifariki kutokana na tatizo la moyo kufeli na kushindwa kufanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoani hapa, Kamanda muroto amesema kabla ya kifo chake mnamo tarehe 21,Disemba,2019 alihudhuria mkutano wa mahusiano ya  dini mbalimbali huko Jijini Dar es salam na kurejea Dodoma tarehe 22 Disemba,2019 kwa kutumia usafiri wa basi la kampuni ya kimbinyiko na Baada ya kufika Dodoma alifika ofisini kwake Mtaa wa Barabara ya Nyerere,kata ya madukani, akiwa ofisini kwake alipatwa na tatizo la moyo kufeli hivyo alifariki kutokana na kukosa msaada wa haraka.

Wakati huo huo Kamanda muroto amesema kutokana na safari yake hiyo alikosa mawasiliano na ndugu zake baada ya simu yake kuzima na kwa kuwa ndugu zake walifahamu amesafiri waliendelea kumtafuta kwa njia ya simu bila mawasiliano.

Amesema Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na wataalamu wa uchunguzi wa matuko kuchunguza tukio hilo ambapo eneo la tukio lilifanyiwa uchunguzi na upekuzi katika ofisi yake na kugundua kuwa hakukuwa na uharifu wowote ,hakuna wizi kwani upekuzi ulifanyika na kukutwa begi dogo lenye nguo chache za safari ,simu yake ikiwa imezima,tiketi ya safari,pesa katika wallet shilingi laki mbili na sitini (260,000) na vitambulisho vyake.

Katika hatua nyingine amesema mwili wa marehe ulipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na kufanyiwa uchunguzi na Daktari na kuthibitisha kuwa sababu ya kifo chake ni moyo kufeli na kushindwa kufanya kazi (Cardial Arrest).

Hatahivyo, ametoa wito kuwa watu wasitumie taarifa za kifo hicho kupotosha umma au kuunda taarifa zenye upotoshaji kama ambazo zinaenezwa mitandaoni.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: