Mwenyekiti wa shirika  lisilo  kuwa  la  kiserikali  linalo jihusisha na masuala   ya  usaidizi  wa  kisheria katika manispaa  ya  Iringa (IPACE) Isaac Kikoti akiongea wakati wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na wanahabari kuhusiana na ukatili wa kijinsia 
Baadhi ya washiriki wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi,wadau mbalimbali na baadhi ya wanahabari

 FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuheshimu haki zote za mtoto ili kuepukana na ukatilii unaendelea kwa watoto kwa kuwalea katika malezi mazuri yenye faida katika maisha ya baadae.

Hayo yamezungumzwa na afisa wa dawati la jinsia  na watoto Elizabert Swai wakati wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na wanahabari kwa uratibu wa shirika  lisilo  kuwa  la  kiserikali  linalo jihusisha na masuala   ya  usaidizi  wa  kisheria katika manispaa  ya  Iringa (IPACE).

Swai alisema kuwa wenye viti, wapya waliopishwa hivi karibuni wametakiwa kuzifikisha tuhuma zozote za ukatili wa kijinsia katika dawati la jinsia la jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi. 

Alisema kwamba matukio ya ukatili wa jinsia yamekuwa yakiongezeka na watu wa Kwanza kukutana nayo ni wenyeviti wa mtaa hivyo ni muhimu kufikisha hatua za mbele,watoto wengi wamekuwa wakibakwa au kunyanyaswa kijinsia.

Aidha Swai ametoa wito kwa watu wanaokumbana  na matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji kujitokeza katika kituo cha polisi ndani ya masaa 72 ili kuweza kufanya upelelezi na kutibiwa kama umeambukizwa magonjwa ya zinaha au ukimwi.

Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa shirika  lisilo  kuwa  la  kiserikali  linalo jihusisha na masuala   ya  usaidizi  wa  kisheria katika manispaa  ya  Iringa (IPACE) Isaac Kikoti alisema kuwa katika siku  16 wamefanikiwa kutoa msaada wa kisheria  kwa wahanga mbalimbali katika jamii ya watu waishio katika manispaa ya  Iringa ,na walio nje ya manispaa  na wametatua migogoro ya ardhi,ndoa ,mirathi ,matunzo ya watoto na ukatili wa kijinsia
“Ndoa na ardhi kesi hizi zimekuwa nyingi katika jamii zimechukua nafasi  kubwa katika jamii ya wananchi wa manispaa ya Iringa na tumefanikiwa kuwasaidia kwa kuwaandikisha wateja wetu katika vitu vya ushauri kama Mahakamani,Polisi,Ustawi wa jamii na Dawati la jinsia manispaa ya Iringa” alisema Kikoti.

Alisema kuwa wamefanya utafiti  kwa  wanao tendewa vitendo  vya ukatili kwa kuangalia maendeleo yao baada ya mashauri yao kutatuliwa na kugundua wana endelea vizuri na wamegundua kuwa elimu iliyotolewa kwa wananchi wanatoa ushirikiano kwa kutoa taarifa. 
“vitendo vya ukatili vime pungua katika jamii kwa asilimia kubwa baada ya watu kupata ushauri kutoka kwa PARALEGAL  na jamii imenufaika baada ya elimu wameweza kujua haki zao za msingi na kuondokana na mila na desturi potofu lakini wanakuwa wazi kupeleka mashauri katika vyombo vya sheria”alisema Kikoti
Lakini pia Kikoti alizitaja changamoto ambazo wamekuwa wanakabiliana nazo ni kutokuwa na usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ili kuifikia jamii kwa ufasaha ,Jamii kutotoa ushirikiano pale ambapo vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinatokea,Mabadiliko ya sheria mpya ya msaada wa kisheria,pindi ambapo kila msaidizi wa kisheria anapaswa kulipa ada Tsh 30,000 kwa mwaka na Taasisi kuto kuwa na mradi wa kujiwezesha.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye semina hiyo mwenyekiti wa kuwasimamia watetezi wa kisheria Tanzania Bara Eliah Kasanga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeanzisha baraza watetezi wa kisheria kwa lengo la kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kiuchumi ili nao waweze kupata haki zao.
“Ukifika mahakamani mtafute anayesimamia utetezi wa kisheria utapata msaada wa kisheria,maana ya mheshimiwa Rais ni kwamba mtu asifungwe kwa sababu hana uwezo ila ufungwe kwa sababu unakosa nah ii sheria ipowazi inapswa kusambazwa kwa wenyeviti wote mkoani hapa ili kwasaidia wananchi kupata haki zao” alisema Kasanga
Na afisa utamaduni wa manispaa ya Iringa Merysina Ngowi alisema kuwa watoto wanaofanyiwa ukatilii wamekuwa wanaathirika kisaikolojia kutokana na matendo yanakuwa yamewakumba.
Alisema kuwa watoto wakifanyiwa ukatili wanapata madhara makubwa katika maisha yao hivyo wananchi wanatakiwa kuheshimu haki za watoto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: