Monday, 23 December 2019

HOSPITALI YA RUFAA MBEYA YAJIVUNIA MAFANIKIOMaafisa habari habari wakiwa na mkurugenzi wa hospital Dkt Godlove Mbwanji wa kwanza kushoto waliokaa
Mkurugenzi wa hopitali ya rufaa kanda ya nyanda za juu kusini Dkt. God love Mbwanji akizungumza na timu ya maafisa habari waliochini ya vitengo vya wizara ya afya


Na Esther Macha, Mbeya

HOSPITALI  ya rufaa ya kanda ya  nyanda za juu kusini  imeboresha huduma zake na kuwa na ongozeka
Kubwa la upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 70  mpaka kufikia asimilia 95 baada ya kuanzishwa duka la dawa la bima.

Mkurugenzi wa hospitali ya kanda nyanda za juu kusini  ,Dkt Godlove Mbwanji alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano kwa timu ya tunaboresha sekta ya
afya inayoongozwa na maafisa habari walio chini ya wizara ya afya.

Dkt .Mbwanji alisema kuwa pia wana mpango wa kuanzisha kitengo cha magonjwa yay kansa cha upatikanaji wa dawa ambao utakuwa kwa asilimia 98.

Akielezea zaidi Mkurugenzi huyo alisema kwamba pia kuna ongozeko la madaktari bingwa 36 Kati ya mwaka 2015 mpaka 2019 na kufanya idadi ya madaktari bingwa kufikia 53 ambao wanatoa huduma katika idara mbalimbali .

"Ongozeko hili katika katika kutoa huduma za matibabu yanayohitaji upasuaji kwa siku sita za juma na huduma za dharura pia "alisema Dkt. mbwanji.

Akizungumzia kuhusu kitengo cha lugha za alama alisema kuwa katika miaka minne serikali ya awamu ya tano imeweza kuanzisha huduma ya mkalimani wa lugha ya alama kwa mwaka 2018 hivyo kufanya hospitali ya kanda kuwa pekee nchini Tanzania kuanzisha huduma hiyo.

Alisema huduma hiyo ilianzishwa baada ya kuona watu wenye ulemavu kutosikia kushindwa kupata huduma Swahiki za matibabu kutokana na kukosekana kwa mawasiliano Kati ya mgonjwa na daktari  pamoja na watoa huduma wengine.

Hata hivyo alisema katika kutoa huduma hiyo mpaka sasa wameweza kuhudumia wagonjwa 22 wa kawaida kwa siku wenye ulemavu wa kusikia 27.

Alisema kwamba klinki ya madawa ya kupunguza makali ya VVU, na kwamba watu 12 tayari wamefanyiwa upasuaji mdogo  na mkubwa ikiwemo uvimbe  kwa akina mama 16 ,pia wameweza kufanyiwa tohara 7 na wengine wanahudhuria klink ya wazazi.


No comments:

Post a comment