Thursday, 26 December 2019

Askofu Gavile asoma salamu za mkuu wa KKKT za Sintofahamu ya uchaguzi

Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Mchungaji Blaston Gavile akitoa salamu za mkuu wa kanisa hilo 
 
Waimbaji wa Kwaya kuu KKKT usharika wa kanisa kuu Iringa wakiwa katika ibada ya Krismasi
Wanakwaya wa Kwaya kuu 

Wanaimbaji kwaya ya watoto na vijana 
Mwalimu Jimson Sanga akiongoza kwaya Kuu 
Askofu Blaston Gavile akisalimiana na muumini wake 
Mwalimu Lupyana Samweli akiongoza kwaya ya vijana 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana akinunua kitabu 
Askofu Gavile akisalimiana na waumini wa kanisa kuu
Maandamano ya waumini wa kanisa kuu wakiongozwa na kwaya kuu 
Balozi Pindi akisalimiana na waumini Iringa 
Balozi Dkt Pindi akisalimiana na muumini wa kanisa kuu 
Msaidizi wa askofu KKKT dayosisi ya Iringa Askali Mgeyekwa 
Waumini wakisalimiana 
Kwaya ya tarumbeta 
Askofu wa kanisa la kiinjili kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akimpongeza mkurugenzi mpya wa muziki dayosisi ya Iringa Jimson Sanga
Askofu Gavile akisoma ujumbe wa mkuu wa kanisa hilo
             Mahubiri yakiendelea
Askofu Gavile akisisitiza jambo wakati wa mahubiri
Waumini wakifuatilia mahubiri ya Krismasi
 
Askofu Gavile kulia akizungumza na mmoja wa waumini wake pamoja na wasaidizi wake


Kanisa   la  kiinjili la  kilutheri  Tanzania  (KKKT) limesema kutokana na sintofahamu  iliyojitokeza  katika uchaguzi wa  serikali za  mitaa uliofanyika bila kuwepo  muafaka wa pamoja  kwa wadau mbali mbali  muhimu vikiwemo  vyama vya siasa na  taasisi  nyingine kwa  sasa  kila mmmoja anahitaji habari  njema ya  furaha  kuu 

Huku  balozi wa Tanzania  katika jamhuri ya  watu wa Kenya Dkt  Pindi  Chana akiwataka  watanzania  kuendelea  kulinda amani na uzalendo kwa Taifa  kwani kazi inayofanywa na Rais Dkt  John  Magufuli ya kuliletea Taifa  maendeleo ni  kubwa kila mmoja  azidi  kumuombea  Rais  ili taifa  liendelee  kuwa ni taifa la mfano kwa nchi  za Afrika kwa amani na kasi ya maendeleo .

Akiwasilisha jana mbele ya waumini wa usharika wa kanisa kuu salamu za mkuu wa kanisa hilo Dkt Frederick Shoo  ka  usharika  wa kanisa  kuu ,askofu wa KKKT Dayosisi ya  Iringa Blaston  Gavile  alisema  kuwa salamu  hizo  anazisoma kama  zilivyotumwa na mkuu huyo wa kanisa kwa nchi nzima .

“Malaika  akawaambia ,msiogope  kwa kuwa  mimi  ninawaletea habari  njema  ya  furaha  kuu  itakayokuwa kwa  watu  wote ( Luka 2;10) kwanza kabisa  naomba    tuungane   wote  kwa   unyenyekevu na  kuimba  sifa  na shukrani nyingi kwa   Mungu  wetu  aliyetulinda  tangu tulipouanza  mwaka huu wa 2019  na  sasa  tunaelekea  mwisho wake  hakika  tumeona mkono  wa  Mungu ukitenda  kazi katika  maisha  yetu  ni kwa neema  ya  Mungu kwamba  tumevushwa  katika  mengi magumu  hadi kufikia kipindi cha majira  haya  wakati   huu wa mwaka “ alisoma  askofu  Gavile .

Kuwa  katika  mwaka   huu  ambao  unakwenda kumalizika   sasa  ni  wazi  kwamba  haukuwa mteremko na raha  tu ,bali  kumekuwa na changamoto nyingi za kimaisha  na  wapo  waliouguliwa   sana na  wengine hata  kuondokewa na  wapendwa  wao  na  baadhi yao  kupata  wakati mngumu  hata jinsi ya kulipa gharama  za elimu ya  watoto pamoja na  kuwapatia mahitaji  mengine muhimu  imekuwa  ngumu  kutokana na changamoto za kiuchumi .

Alisema  mwaka  huu pia tumepata  kushuhudia  uchaguzi wa  serikali za mitaa na  vijiji ukifanyika  kama kawaida  ilivyo kwa  nchi  nyingi za Afrika  uchaguzi  huo haukupita  bila   changamoto   kwani  wamepata kushuhudia sintofahamu  kadhaa katika mchakato mzima   jambo lililosababisha  kuingia katika uchaguzi huo bila changamoto hizo  kufikiwa  muafaka .

  Mwaka huu nimechagua neno  kutoka injili ya Luka  inayosema   tunamsikia malaika akitangaza  habari njema  ya furaha  kuu ,habari hii  hakika  ni  ya furaha  kuu 
maana  ni ya kweli na  haina ubaguzi  ni kwa watu  wote “

Alisema habari ya kuzaliwa  kwa  Mwokozi wetu  Yesu Kristo  ni habari njema   nay a  furaha  kuu kwa  watu wote  yaani matajiri  na masikini  yatima na wajane  ,wasomi na  wasio wasomi   ,tangazo la malaika  linatutaka  wote kusahau  changamoto  na magumu yote tuliyokutana  nayo  mwaka  huu na kumtazama yesu  Kristo  mwakozi wetu  anayetuletea furaha  kuu  mioyoni mwetu  na maishani mwetu  kwa  ujumla .

Kuwa   furaha  kuu ya kwanza ambayo inapaswa kupokelewa  katika  neon  ni kwamba Mungu anatupenda na ndiyo maana  amemtuma mwanae wa pekee aje  kutukomboa toka dhambini  kuwa  hiyo ni furaha  yakweli kwa  watu  wote na sasa hakuna atakayepotea tena  kwani  nuru  imekuja  ulimwenguni  na kupitia  hiyo Nuru yaani   Yesu kristo  ni  wazi  tumeahidiwa  uzima  wa  milele baada ya  kusafishwa dhambi zetu  ilieleza  barua   hiyo ya Dkt  Shoo.

Kwa  upande wake balozi  wa Tanzania nchini Kenya  Dkt  Pindi  Chana  alisema  kuwa  Tanzania  imekuwa ni nchi ya kuigwa  na mfano miongoni mwa nchi  za Afrika kwani  kwa  Kenya wengi  wanafurahia   sana  demokrasia  ya Tanzania na uzalendo wa watanzania katika nchi yao .


Dkt  Chana  alisema  watanzania waliopo Kenya  wanampongeza sana Rais Dkt  John Magufuli kwa  kuisimamia  nchi   vizuri na hata  kuifanya  nchi  kuwa na maendeleo  makubwa  jambo ambalo  linawavutia  wengi .

  watu  wengi  wanajifunza mambo  mengi sana kutoka  Tanzania   hasa juu ya amani na Imani kwa  kila mmoja  kuabudu kwa  uhuru  Zaidi  ikumbukwe  mwalimu baba wa Taifa aliweza  kuliunganisha Taifa  vizuri na kulifanya kuwa taifa  lenye amani na upendo ila pia Rais Dkt Magufuli ameendelea  kuenzi  yote ya baba wa Taifa “

Dkt  Chana  alisema ujumbe wake kwa  niaba ya   watanzania  wanaoishi nchini Kenya ni  kuendelea  kuhimiza  watanzania  kutunza mazingira kama ambavyo  serikali ya Tanzania  ilivyoweza  kuthibiti matumizi ya mifuko ya plastiki  kuwa  kampeni   hiyo itawezesha  mazingira  kuwa  safi na bora .

No comments:

Post a comment