NA HERI SHAABAN

WANAFUNZI 20 wa Mkoa wa Dar es Salaam wamefanya vizuri katika  mashindano ya Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK)

Mashindano hayo ya KKK ngazi ya Mkoa wa Dar es Salam yameshirikisha wanafunzi wa darasa la kwanza na darasa pili pamoja na  kuwatambua Walimu mahiri wa KKK wa mwaka 2019.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi za wanafunzi 20 waliofanya vizuri na walimu wao Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu alisema katika mkoa huo sekta ya elimu msingi anajivunia kitaaluma wapo vizuri

Lisu alisema mwaka wa tatu mfurulizo katika matokeo ya darasa la saba kitaifa mkoa huo unashika nafasi  ya kwanza .

"Katika mkoa wangu nina walimu mahili hii ni sehemu ya kujivunia  kwasasa pia tumefanya vizuri katika Mwenge wa Uhuru mwaka huu Dar es salaam tumeshika nafasi ya kwanza ,kuandikisha zoezi la wapiga kura nafasi ya kwanza "alisema Lissu


Aidha alisema mashimdano hayo ya KKK awali yalianzia ngazi ya kata  ,wilaya mpaka  sasa yamefikia mkoa washiriki watashiriki  mashindano ya Kanda ngazi ya Taifa.

Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma Mkoa huo Janeth Nsunza alisema mashindano hayo pia yameshirikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum na walimu wao kutoka wilaya zote tano.

Janeth alisema kila wilaya wamechukua wanafunzi wanane wamepambanishwa na kupata wanafunzi bora katika Mahiri za KKK ambapo wanafunzi walipewa vifaa vya shule na vyeti kwa upande wa  Walimu wao walipewa motisha kwa msindi wa kwanza mpaka wa tatu.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: