Jana tarehe 10/11/2019 historia iliendelea kuandikwa katika katika Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani katika mkutano mkuu wawajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya mkuranga ikiwa sambamba na taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Kwa miaka minne wilayani humo,

Ni Naibu waziri wa Nishati na umeme mh Subira mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani ambaye aliitangaza vyema na kuwashibisha wanamkuranga juu ya serikali ya Awamu ya Tano ikivyofanya makubwa kwenye secta ya umeme Kwa kipindi hiki cha miaka minne Chini ya Rais John pombe Magufuli na kuwataka wanamkuranga kutulia kwani serikali Yao iko makini kwenye utendaji kazi,
Mh Subira mgalu alisema kuwa kipindi serikali ya Awamu ya nne inaingia madarakani wilaya ya mkuranga ilikuwa na Umeme vijiji 20 Jambo ambalo secta hiyo imepiga hatua na na kuongeza 36 huku vijiji vingine vilivyosalia viko kwenye mkakati wa kuingiziwa umeme kwenye mzunguko unaofuata, pia mh mgalu aliongeza kuwa kufikia mwaka 2021 vijiji vyote Nchi nzima vitakuwa vimefikiwa na Umeme kwani serikali imejipanga kikamilifu kutekeleza Ahadi zake Kwa wakati,

Naye Naibu waziri wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi mh Abdala Hamis Ulega aliwataka wajumbe hao waliojitokeza Kwa wingi siku hiyo ambao ni zaidi ya 2100 na kuwasomea utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi katika Jimbo Hilo Kwa kutaja maendeleo ya Elimu ikiwa na ujenzi wa Shule za msingi na Sekondari ambazo zimejengwa Kwa Kasi ya ajabu Sana kila kijiji tofauti na awali,pia mh Ulega aliishukuru Wizara ya Nishati na umeme Kwa utekelezaji wao wa kuwaunganishia umeme wanamkuranga Kwa Kasi ,

Pia Naibu waziri wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi mh Abdallah Ulega hakusita kuongelea suala la miundo mbinu wilayani humo, ambapo aliwaeleza wajumbe kuwa kwenye miundo mbinu tuko vizuri hasa kwenye Bara Bara za hapa mjini Ila kero kubwa ni Bara Bara za vijijini ndizo zenye Changamoto kubwa na kumtaka manager wa TANROAD wilayani humo kushughulikia haraka kwani wanamkuranga wanahitaji maendeleo na si vinginevyo kwani pesa zipo hivyo hakuna kulala ,

Pia mh Abdallah Hamis Ulega hakusita kuongelea kuhusu maendeleo ya Hospital ya wilaya ya mkuranga (mkwalia) ambapo hapo Mwanzo haikuwa na X-RAY machine wala Kipimo cha Utra Sound ambapo hivi sasa serikali ya Awamu hii ya Tano inayowajali wananchi wake imetekeleza machine hizo na zinafanya kazi, hivyo wananchi wa mkuranga hawaendi Dar es salaam kupata huduma hizo kama hapo Mwanzo,

Pia mh Abdallah Ulega hakusita kuongelea Changamoto za hospital hiyo kuzidiwa na Wagonjwa wengi hasa wengi wao si wakazi qa eneo la mkuranga,

"Mh mgeni rasm hivi sasa mkuranga wakina mama zaidi ya 300 wanajifungua Kwa mwezi tofauti na Mwanzo ambao idadi Yao ilikuwa ni 80 ,na ukifuatilia wengi si wakazi wa mkuranga Bali wanatoka maeneo mengine hasa mbagala, zakhiem nk jijini Dar es salaam hivyo tunaomba kusaidiwa zaidi ili hospitali hii iweze kujimudu"-  mh Abdallah Ulega

Pia mh Abdallah Ulega alimtaka mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa NEC KANALI mtaafu NGEMELA LUBINGA kufikisha salamu za wanamkuranga Kwa mh Rais Magufuli kuwa wananchi wa mkuranga wanampenda na pia wanakipenda Sana Chama cha mapinduzi (CCM)

Vile vile mh Abdallah Ulega katika mkutano huo mkuu wa wajumbe wakiambatana na wagombea wote wa vitongoji na vijiji alifanikiwa kugawa Spika kila kata na pesa zaidi ya shs 10 mil zigawanywe katika kila kata kwaajili ya kusaidia Changamoto mbali mbali kuelekea  katika kilele cha Uchaguzi wa serikali za mitaa.
#mkuranganaabdallaulega
#uzalendokwanzakwamaendeleoyataifa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: