Friday, 29 November 2019

RIDHIWANI ATAFUNA MFUPA ULIOWASHINDA WENGI

MBUNGE wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kuwapa heshima ya uhakika wa kufanikiwa kwa wananchi wa jimbo lake.

Mfupa huo uliwashinda watangulizi wake katika jimbo hilo ni kufanikiwa kwa kupata kwa hati miliki za maeneo kwa baadhi ya wanachalinze mara baada ya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi hao. 

Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano ya hati kwa wale waliokamilishi kulipia hati hizo Kikwete alisema kuwa hati ni muhimu sana kuwa nayo kwani mbali na kukopesheka unakuwa umepandisha thamani ya kiwanja chako. 

"Nimefurahishwa sana kwa kitendo cha wananchi wangu kupata hati za viwanja vyao kwani huu ni mwanzo wa mafanikio katika maisha yao"Alisema Kikwete.

Aidha ameipongeza kamati ya watu 12 iliyoundwa kwa ajili ya kuhamasisha wananchi waweze kujitokeza kupimiwa maeneo yao ili yaweze kupanda thamani ya ardhi."Nimefanikiwa kukabidhi hati 48 kwa wananchi Δ·ati 100 waliolipia hivyo ni wakati wa kuchangamkia fursa hii ili kuondokana na kuwa na maeneo ambayo hayajapimwa"

Aluongeza kuwa katika kata ya Bwilingu mpaka sasa viwanja 10000 vimepimwa na wananchi wapo kwenye mchakato wa malipo ili nao waweze kupatiwa hati.Hivyo sasa chalinze itaingia kwenye moja ya halmashauri zitakazoongezea kipato serikali kupitia kodi za ardhi.

Pia ametoa wito kwa wananchi wake kuendelea kujitokeza ili waweze kupimiwa maeneo yao.Naye mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji na hamasa kwa wananchi Shamba Msakamali amempongeza mbunge kwa ushirikiano wake wa dhati katika kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwenye zoezi.

Msakamali aliongeza kuwa msaada uliotolewa na mbunge Kikwete ni mkubwa na wenye tija kwa wanakamati.Kwa upande mwanana Ally ambaye ni miongoni mwa wale waliokabidhiwa hati alisela kuwa watu wamekuwa wakikata tamaa juu ya mwenendo wa awali kwa ajili ya upatikanaji wa hati.

Hivyo amewataka wananchi kujitokeza ili nao waweze kupata hati zao kama wengin nye.


No comments:

Post a comment