KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akigawa sehemu ya bidhaa ambazo zilikamatwa na kutaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha ambazo ni sukari mifuko 278 na mafuta ya kupikia madumu 1241na hivyo kamisha wa Idara ya forodha na Ushuru wa Bidhaa ameamua kutoa kama
msaada kwa taasisi mbalimbali hususani vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na magereza kwa mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamisha Msaidizi wa Jeshi la Magereza Emanuel Lwenga
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakikagua vitu hivyo kabla ya kugawa kwa walengwa
 Sehemu ya bidhaa ambazo ziligawiwa ambazo ni mafuta ya kula 
 Sehemu ya sukari ambayo iligawanywa leo
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said amewaonya watumishi wa umma mkoani humo kuacha kujihusisha na masuala ya magendo huku akiwaambia kwamba kufanya hivyo ni kudhoofisha juhudi za serikali kukusanya mapato.

Mhandisi Zena aliyasema hayo leo wakati akikabidhi msaada kwa magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye mahitaji maalumu na vuti vya kulea wazee ambavyo vimetolewa na Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA nchini kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 217(2)(a) cha sheria za forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki cha mwaka 2004.

Kupitia kifungu hicho Kamisha huyo ameamua kutoa msaada ya vyakula ambavyo ni sukari na mafuta ya kupikia kwa magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye mahitaji maalumu na vituo vya kulea wazee

Vyakula hivyo vinatokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa.

Alisema kwamba lazima watumishi hao wa umma wawe mstari wa mbele kuwafichua watu wanaohusika na biashaza magendo badala ya kushirikiana nao katika kuingiza bidhaa hizo kwa njia za panya ambapo wanachangia kuikosesha serikali mapato ambayo ndio yanasaidia kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa wananchi.

“Ndugu zangu watumishi wa umma jiepusheni na magendo na anzeni kuwafichua wanaoingia magendo na wananchi endelee kutoa taarifa kwani tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kumaliza kabisa suala la biashara za namna hiyo “Alisema Ras Mhandisi Zena.

Hata hivyo Katibu tawala huyo aliipongeza mamlaka hiyo kwa kujielekeza kwa taasis hizo kwa kuzipa ahueni kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa waledi kwenye kukamata bidhaa hizo.

“Bidhaa hizo zimekatwa kwa sababu zilitakiwa kulipa kodi ya serikali imeshindikana na kama zingekuwa zimepita kinyemela zingeipa hasara serikali hivyo niwapongeza TRA kwa  na Kamishna wa Forodha kwa kufanya kazi kubwa na nzuri kupambana na vitendo vya namna hiyo”Alisema

 Awali akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitu hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA) Speciaoza Owure alisema kwamba mzigo huo ulitaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha hivyo kamisha wa Idara ya Forodha kuamua kutoa msaada kwa taasisi mbalimbali.

Alizitaja taasisi hizo ni vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na Magereza ambao waligawiwa vyakula hivyo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi katika halfa iliyofanyika mjini Tanga

“Kwa niaba ya Kamisha wa Forodha tunaomba uridhie kugawa vyakula hivyo vinavyotokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa”Alisema Meneja huyo wa TRA Mkoa wa Tanga.

Alizitaja bidhaa ambazo ziligawiwa ni mifuko ya sukari 278 yenye ujazo wa kg 50 ambazo thamani yake ya kiforodha ni milioni 12.7 na kodi ya forodha ilitakiwa kuwa milioni 12,791,391.60 na VAT milioni 4,604,900.97 .

Aidha waligawa pia madumu 1241 ya mafuta ya kula yenye lita 20 kila mmoja thamani yake ya forodha ni milioni 43, 191, 652.14 na ushuru wake ni milioni 15,117,078.24 na VAT yake ni milioni 10,495,571.44 kwa hiyo thamani ya vifaa vilivyogawiwa ni vyenye thamani ya bilioni milioni 55,983,043.74 zenye thamani ya ushuru wa forodha miloni 27,908,469.84 na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ni  miloni 15,100,472.41.

Hat hivyo alisema vifaa vyote hivyo ambazo viligawiwa vilikuwa na thamani ya milioni 55,983,043.74 na kodi ni sh.milioni 43,008,942.25.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Magezera Mkoa wa Tanga Kamisha wa Msaidizi Emanuel Lwenga alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo kutokana na wao kuwa na wanawahitaji wengi jumla ya wafungwa 1508 wote wanahitaji kupata chakula.

Alisema hivyo wanashuruku kiasi walichowapatia ambapo sukari wamepata jumla ya kilo 9400 na hivyo itasaidia kuwalisha wafungwa kwa kipindi cha miezi sita mkoa wa Tanga mzima huku mafutaa kilo 17442 waliokabidhiwa itasaidia kuwalisha wafungwa mkoa mzima kwa mwaka mzima.

“Lakini pia nitoe wito kwa wakati mwengine msisite kutuma msaada kwani bado tunauhitaji mkubwa kwani wafungwa bado wapo na wataendelea kuwepo hivyo misaada ni muhimu sana kwao “Alisema .
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: