Saturday, 23 November 2019

GURU YAANDA MAFUNZO BURE TABATANA HERI SHAABAN

KAMPUNI ya Guru Planet imeandaa mafunzo bure kwa ajili ya kujifunza kuwezesha kupata  mkopo  wa kuendeleza biashara  yako.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Guru Planet Nickson Martin alisema mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwa muda wa miezi sita  ufunguzi wake  kuanza Novemba 23 mwaka huu makao Makuu ya Guru Planet, Tabata Wilayani Ilala.

" Tumeandaa Kliniki ya Biashara ya Guru Planet  kwa ajili ya kutoa fursa kwa wajasiriamali,Makao Makuu ya Guru Planet mawasiliano 0758061582 mafunzo haya kwa washiriki yatakuwa bure  wajasiriamali wanaofanya vizuri watawezeshwa mikopo yenye masharti nafuu kutoka taasisi ya fedha  ya Wajasiriamali Microfinance PLC "alisema  Martin.

Martin alisema mafunzo yanalenga maeneo matatu ,mafunzo kwa wajasiriamali ambao wanataka kuandaa Biashara,mafunzo kwa wasimamizi wa biashara,mafunzo ya kuendeleza biashara  .


Alisema dhumuni la mafunzo hayo ni kusaidia wajasiriamali kufanya biashara yenye tija na kuwawezesha kupata mkopo wa kuendeleza Biashara yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano John Magufuli  katika kujenga Tanzania ya uchumi wa  viwanda.

Aidha alisema WAJASIRIAMALI MICROFINANCE PLC ni Taasisi ya umma na inamilikiwa na wajasiriamali wenyewe pia inatoa fursa ya wajasiriamali hao kuwekeza  ndani ya taasisi. Mafunzo tunatarajia yatatatua changamoto za kukopa na kushindwa kurejesha.


 Guru Planet Ltd ni Kampuni inayohusika na kutoa ushauri elekezi na ni mdau wa maendeleo. Ilipewa kibali cha kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala na kutatua changamoto za masoko ili kuwakwamua wajasiriamali kiuchumi.

MWISHO
Tabata Novemba 22/2019

No comments:

Post a comment