NA HERI SHAABAN

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo jana amezindua mradi wa maji safi na salama kwa wakazi wa Marui Mipera Wilayani Kisarawe.


Mradi huo wa Maji umfadhiliwa na Shirika la Reflection Foundation  (ARF)kwa kushirikiana na Ghulam Hussein Electra Chertable .

Akizindua mradi huo Joketi alitoa onyo kwa watumiaji maji hayo wasitumie kama chanjo cha Biashara  kwakujinufaisha wao mradi huo ni kwa ajili ya jamíi nzima.


"Zaidi ya wakazi 4000 wa kijiji ichi Marui watanufaika na mradi huu wa maji serikali yetu sikivu imewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji tunawashukuru wafadhiri wetu  waliowezesha mradi huu "alisema Joketi.

Joketi alisema mradi huo ni mkubwa mpaka ukikamilika utakuwa  umegharimu shilingi milioni 69 chini ya ufadhili wa Reflection Foundation (ARF)kwa ushirikiano wa Ghulam Hussein Erectra Charitable.


Alisema alisema katika kijiji hicho kwa sasa kero imekwisha mradi huo ukikamilika kisima kina urefu wa mita 200 .

Katika uzinduzi wa mradi Mkuu wa Wilaya Joketi Mwegelo alikabidhiwa na
Balozi wa shelisheli ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Afrika Reflection Foundation (ARF) MERY VAN POOL pamoja na mkurugenzi Taasisi  Ghulam Hussein NAFEESA JANMOHAMMED.





Share To:

msumbanews

Post A Comment: