WIZARA ya Fedha na Mipango imtangaza kuwa sasa mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi umezinduliwa rasmi huku ikisisitiza kuwa wakaguzi wa ndani wa taasisi za umma wataanza kuutumia mfumo huo kikamilifu na kuachana na utamaduni wa kuwalisha taarifa za ukaguzi kwa mlipaji mkuu wa Serikali kwa kutumia nakala ngumu.

Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa mfumo huo leo Oktoba 31 jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango aliyekuwa mgeni rasmi Amina Shaaban amesema kuwa mfumo huo utafanyiwa maboresho ili kuwaingiza wadau wengine wa umma walio katika ofisi ya Msajili wa Hazina, wasimamizi wa wakaguzi wa ndani na mamlaka za Serikali za Mitaa walio katika sekretarieti za mikoa TAMISEMI na hata wakaguzi wakuu ili kurahisisha utendaji kazi serikalini.

Pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo kutenga fedha kupitia idara ya mkaguzi wa ndani mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha mfumo huo  kuhakikisha kuwa watumiaji wote wanapata mafunzo stahiki ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza bado kuna watumishi wengi hawana mafunzo kuhusu mfumo huo na hivyo wataendelea kuelimishwa siku hadi siku.

"Nipende kumshukuru Kaimu Mkurugenzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kwa kunialika katika kuzindua mfumo huu muhimu wa kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi katika taasisi za umma(GARIITS).Natambua mkaguzi mkuu wa ndani wa Serikali na wataalam wake kwa jinsi walivyoonesha umuhimu wa suala hili na kuhakikisha kuwa wanasaidia mfumo huo wa kieletroniki wa kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya wakaguzi wote wa ndani na nje yanayotolewa kwenye taarifa zao za mara kwa mara. Pia natambua sheria ya fedha ya mwaka 2010 iliweka jukumu la kumsaidia mlipaji mkuu wa Serikali katika ya ukaguzi wa ndani katika masuala ya ukaguzi wa ndani katika taasisi zote za umma,"amesema Shaaban.

Amefafanua kuwa kuwamoja ya lengo kuu katika mpango mkakati wa Wizara ya Fedha na Mipango wa mwaka 2017-2022 ni kuimarisha usimamizi wa masuala ya fedha na uwajibikaji , hiyo inajumuisha kuimarisha mifumo ya kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa ndani na wakaguzi wa nje wa taasisi zote za umma.

Aidha amesema Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma kupitia kufanya tathimini ya utendaji."Kwa mantiki hii wakaguzi wa ndani katika taasisi zote za umma wanatakiwa kutekeleza wajibu wa kuthamini na kutoa taarifa za utekelezaji wa mapendekezo yaliyo katika taarifa za ukaguzi zilizotolewa na wao hata zile zilizotolewa na wakaguzi wa nje na maelekezo yanayotolewa na waangalizi wengine kama mamlaka za usimamizi na kamati za Bunge,"amesema.

Pia amesema ikumbwe kwamba Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa kuishia mwaka 2025 unasisitiza kuhusu  utawala bora ni msingi muhimu na uwekaji wa utamaduni wa uwajibikaji.Utawala bora ni msingi muhimu katika kusuma mbele ajenda ya maendeleo ya nchi yetu.

Hata hivyo amesema ili kuwezesha utekelezaji kikamilifu wa mapendekezo yaliyotolewa katika taarifa za ukaguzi katika mnyororo wa uwajibikaji na usimamizi bora wa masuala ya fedha ni wazi kuwa Serikali ilihitaji mfumo madhubuti wa kukusanya taarifa sahihi za mapendekezo ya wakaguzi yaliyotekelezwa na mapendekezo ambayo hayajatekelezwa kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi.

"Mfumo huu ambao nimeuzindua utakapatikana kwa njia ya mtandao mahali popote alipo mkaguzi wa ndani wa taasisi za umma , utakuwa rafiki katika kuutumia , utaweza kuboreshwa bila kutumia gharama kubwa na kuwaongeza watumiaji wengine watakaoonekana ni muhimu na hauna gharama za mara kwa mara za leseni,"amesema Shaaban.

Ameongeza anazo taarifa kuwa pamoja na kuwa na Serikali inao wakaguzi wa ndani zaidi ya 1,200 ni wakaguzi wakuu wachache tu wasiozidi 200 waliopatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo huo na ambao kwa sababu wanautumia kuwalisha taarifa zao kwa mlipaji mkuu wa Serikali.Pia amesema amefuatilia mfumo huo bado unachangamoto chache zilizojitokeza baada ya kuutumia kwa majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni kutotambua  wadau muhimu kama maofisa masuuli, wasimamizi wa mashirika ya umma walioko katika ofisi ya Msajili wa Hazina, wasimamizi wa wakaguzi wa ndani.Hivyo ni matarajio yake baada ya uzinduzi huo changamoto hizo zitapata ufumbuzi wake kwa mfumo kufanyiwa marekebisho ili kuwaungiza wadau wengi zaidi. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban akizungumza mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani), leo jijini Dar wakati wa kuzindua rasmi mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa Taarifa za ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information Tracking Systtem-GARIITS). Wageni waalikwa hao pia Washirika wa Maendeleo  kupitia mpango  wa kuboresha  usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mhandisi Amin Mcharo akieleza namna ya kutumia mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa Taarifa za ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information Tracking Systtem-GARIITS) mbele Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi Amina Shaaban na Wageni waalikwa mbalimbali ambao ni Washirika wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo.
Sehemu ya Washirika wa Maendeleo kupitia mpango wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),wakifuatilia aliyokuwa akizungumza mgeni rasmi kuhusiana na mpango huo muhimu kwa Serikali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban  (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Washirika wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: