Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) Dkt Margaret Mollel amewataka wauzaji na wasambazaji wa viuatilifu nchini kuepuka uuzaji wa viuatilifu ambavyo vinaingizwa kwa njia za panya ambavyo havijakuguliwa na kusajiliwa na taasisi hiyo ili kuepuka

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu inayofanyikia katika taasisi hiyo hapa mkoani Arusha,ikiwakutanisha  watafiti wa wanaofanya majaribio ya kuhakiki viuatilifu kabla ya kuvisajili kutoka katika vituo vya kilimo hapa nchini pamoja, SUA,TPRI na wataalamu waliobobea katika maeneo hayo ili kuondoa changamoto ya uandaaji wa ripoti.

 Dkt Mollel ametoa wito kwa wafanyabiashara wa viuatilifu kuacha Kufanya biashara bila kibali, Kuuza/kusambaza viuatilifu visivyosajiliwa,Kuuza /kusambaza viuatilifu visivyo na vibandiko (lebo), Kuuza viuatilifu vilivyoisha muda wa matumizi, Uhamishaji wa viuatilifu (Repacking/Decanting)

Kuuza viuatilifu kwenye eneo ambalo halijakaguliwa na Mkaguzi wa Viuatilifu, Kuuza viuatilifu kwa kutembeza mitaani,Kuuza viuatilifu kwenye masoko,  minadani na kutandaza barabarani/vijiweni.Kwani hayo makosa yote yanaweza kusababishia wakulima hasara kwa kununua viuatilifu ambavyo havikidhi haja yao na wakati mwingine kuleta madhara katika mazao, mazingira na hatakwa binadamu.

Aidha amewaasa pia wakulima kuacha kununua viuatilifu  ambavyo vinaingizwa hapa nchini kinyume na sheria vikiwa havijafanyiwa utafiti na kusajiliwa na TPRI  kwa kisingizio cha kupunguza gharama kutokana na wahalifu hao kuuza kwa bei rahisi.

‘’tunataka viuatilifu vilivyo bora hapa nchini, wachukue viuatilifu vyenye nembo ya TPRI ambavyo tumeshakwisha kuvifanyia utafiti,kuvikagua na kuhakiki kuwa havina madhara tunawataalamu walio bobea ambao wanapima vile viuatilifu kabla ya kuvisajili kwaajili ya kutumika hapa nchini hivyo mmavyo nunua kwa bei rahisi havina ubora uliokusudiwa utanunua vingi nabado hautaweza kuuwa visumbufu ‘’amesema Dkt Mollel

Pia amesemakuwa watakao kutwa wakiuza au kuvisambaza viuatilifu ambavyo havija fanyiwa utafiti,kukaguliwa na kusajiliwa na TPRI(ambavyo havina nembo ya TPRI)na makosa hayo mengine watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo Faini: Kati ya TShs 10 milioni hadi 100 milioni kwa makampuni makubwa,mtu binafsi faini Kati ya TShs 2 milioni  hadi 10 milioni au kifungo miaka mitatu au vyote,kwa mkosaji sugu Adhabu zilizotajwa hapo juu pamoja na kunyang’anywa kibali cha kufanya biashara ya viuatilifu.

Aidha akizungumzia warsha ya hiyo inayofanyikia katika taasisi hiyo ikiwakutanisha  watafiti wa wanaofanya majaribio ya kuhakiki viuatilifu  kabla ya kuvisajili kutoka katika vituo vya kilimo hapa nchini,SUA,TPRI na wataalamu waliobobea katika maeneo.

Amesema kuwa warsha hiyo imeandaliwa maalumu kwaajili ya kuondoa changamoto iliyokuwepo katika uandaaji wa ripoti za utafiti ili kukaa pamoja na kuwekeana utaratibu na mwongozo wa namnagani wataandaa ripoti zilizo katika mfumo mmoja pia kwa kufuata miongozo iliyowekwa kwa nchi za jumuia ya Afrika Mashariki.

“ baada ya warsha hii watatoka na mfumo mmoja katika uandaaji wa ripoti,na sio kwamba hapo nyuma walikuwa wanafanya vibaya hapana walikuwa wanafanya vizuri”aliongeza Dkt Mollel

Ametoa wito kwa washiriki wote wa warsha hiyo elimu watakayo ipata waipeleke kwa wengine ambao hawajafanikiwa kushiriki na pia watoke na azimio moja zuri kwasababu itarahisisha katika vikao vya kupitisha viuatilifu kabla ya usajili
Share To:

msumbanews

Post A Comment: