Saturday, 26 October 2019

DC MJEMA AMEMSIMAMISHA MKANDARASI WA KAJENJERENA HERI SHABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemsimamisha Mkandarasi wa usafi Kampuni ya Kajenjere kata ya Buguruni Mnyamani.


Hatua ya kumsimamisha Mkandarasi wa Kajenjere inafuatia wananchi wa Buguruni Mnyamani   kutoa kilio chao kwa Mkuu wa Wilaya wakilalamikia Mkandarasi wa Kajenjere kwa kudaiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kupelekea kata ya Mnyamani kuwa chafu.

" Kuanzia leo namsimamisha Mkandarasi wa kampuni ya Kajengere wananchi wa Mnyamani hawamtaki  Mkurugenzi wa Ilala atampangia kata nyingine kwa ajili ya uzoaji wa taka" alisema Mjema.


Mjema aliwataka wakandarasi wa takataka wanapopewa tenda halmashauri watekeleze majukumu yao ipasavyo ya uzoaji takataka bila kubugudhi wananchi.

Aliagiza halmashauri ya Ilala ipeleke Mkandarasi mpya kata ya Mnyamani na kabla kukabidhi tenda hiyo waitishe mkutano wa wananchi wakubaliane tozo kwa kila kaya kwa  ajili ya kuchangia ada .


Awali kata ya Mnyamani Mkandarasi wa Kampuni ya Kajenjere kila kaya walikuwa wakichangia sh,3000/= lakini taka kampuni hiyo hawazoi kwa wakati hali iliyopelekea wananchi wakatae kampuni hiyo.


Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Damas Parsalaw ameomba apatiwe Mikataba ya Mkandarasi wa Kajenjere ya Kuomba tenda halmashauri ya Ilala ambayo ilimwezesha kufanya kazi ya usafi Kata ya Mnyamani.

Malalamiko yamekuwa makubwa kwa Mkandasi huyu wa Kajenjere  asilimia 90 wananchi wanampinga TAKUKURU Ilala tunaomba Mikataba yake ili tuweze kupitia "alisema Damas.

Wakati huo huo Afisa TAKUKURU Ilala amemwagiza Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto hawachukulie hatua Watumishi wa kata ya Mnyamani kwa kudaiwa kuichafua Serikali.

Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Ilala Asha Mapunda amepiga marufuku Tuisheni katika shule za Msingi halmashauri ya Ilala shule zitakazofundisha tuisheni katika majengo ya shule za Serikali wahusika watachukuliwa hatua.

Asha amewataka wazazi   wazingatie elimu kwa ajili ya kusomesha watoto wao ili Taifa liweze kupata viongozi bora.
Mwisho


No comments:

Post a comment