Thursday, 17 October 2019

BONAH AWAWEZESHA BODABODA KIUCHUMI JIMBONINA HERI  SHAABAN

MBUNGE wa Segerea(CCM )Bonah Ladslaus awawezesha bodaboda wa Tabata Kimanga kwa kuwaunganisha katika vikundi ili waweze kupata mikopo ya halmashauri ya Ilala inayotolewa kwa  Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Bonah aliviwezesha vikundi hivyo vya bodaboda  katika kikao kata ya Kimanga Wilayani Ilala leo,ambapo katika kikao hicho kilichowakutanisha waendesha pikipiki 100 waliunda vikundi kumi vya watu kumi kumi na kuwataka waandae katiba ya kila kikundi kwa watu wanao aminiana.

"Halmashauri ya Ilala kuna fursa nyingi zinatolewa zinawapita mimi kama Mbunge wenu nawaomba muwandae katiba muweze kusajili halmashauri ili muweze  kupata mikopo ya bajaj na boda boda kama mbunge wenu nitawasimamia"alisema Bonah.

Bonah alisema vikundi vyote vitakavyotimiza taratibu na masharti watapewa bodaboda ili waweze kujiali wenyewe badala ya kuajiliwa.


Aliwataka viongozi wa vikundi hivyo kushirikiana na ofisi Mbunge pamoja Mama Maendeleo wa kata katika shughuli za vijana zinazouhusiana masuala ya uwezeshaji kiuchumi .


Alisema mikopo ya halmashauri ya Ilala inatolewa kwa yoyote mradi awe raia wa Tanzania na kufuata taratibu .


Katika hatua nyingine Mbunge Bonah amewandalia utaratibu wa mkopo wa viwanja vya bei nafuu ili waweze kumiliki viwanja vyao wajenge nyumba


Amewataka boda boda wachague na kupendekeza eneo wanalotaka viwanja ofisi ya mbunge Segerea itawasaidia  watakopa watalipa kwa awamu awamu mpaka wanamaliza deni ili waweze kujenga nyumba.

Wakati huohuo amewataka wajiandikishe ili waweze kupata haki ya kushiriki kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali ya Mtaa wenye sifa watakao weza kuleta chachu ya maendeleo na kumsaidia Rais wa awamu ya tano John Magufuli katika utekelezaji wa ilani .


No comments:

Post a comment