Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameongoza zoezi la kuchoma nyavu haramu za uvuvi aina ya KOKOLO na NJENGA zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni miamoja na hamsini zilizokamatwa kwenye operesheni ya uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na wananchi kabla ya kuongoza zoezi la kuchoma vyavu hizo katika kijiji cha Kagongo wilayani mwanga waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina anasema serikali haitamvumilia mwananchi wala kiongozi atakayebainika kuhusika na uvuvi haramu na kuwaita watu hao kuwa ni wahujumu wa uchumi.
Mkuu wa wilaya ya Mwanga Thomas Apson anasema suala la uvuvi haramu mbali na wananchi kuendelea na uhalifu huo pia limegubikwa na sintofahamu hata kwa watendaji wa serikali na kuahidi kuwashughulika bila huruma.
Baadhi ya wananchi walioshudia tukio ilo nao wakapaza sauti zao mbele ya waziri huyo kuhusiana na changamoto wanazokumbana nazo katika mapambano dhidi ya uvuvi huo haramu.
Baadhi ya picha mbalimbali
Post A Comment: