NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KASI ya
ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji
Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya
kutembelea eneo la mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu
ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye mifereji mikubwa ya kuchepusha maji) (diversion
tunnel), pamoja na miundombinu wezeshi ikiwa imekamilika.
Sambamba na
kupigwa kwa hatua hizo muhimu katika utekelezaji wa mradi huo uliozinduliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Julai 26, 2019 na
ambao utazalisha Megawati 2115, pia amepongeza usimamizi na utawala katika
mradi huo.
“Hii ni mara
yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia
masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya
ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt.
Kalemani.
Alisema
baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo
amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima
ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa
ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa
maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na
kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi
nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa
njia za kuchepusha maji ardhini (diversion
tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya
siku 45 na ikamilike. ADIT hiyo yenye urefu wa wa Mita147.6 nashukuru
wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.
Mheshimiwa
Dkt. Kalemani pia alisisitiza kuwa ni matumaini ya serikali kwamba wakandarasi
watamaliza kazi ya ujenzi ndani ya muda na kwamba hakuna muda
utakaoongezwa.
“Nimatarajio
yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu pia watatukabidhi mradi
huo siku hiyo saa 9;30 alasiri ili na mimi niukabidhi kwa Watanzania.”
Alisisitiza na kuongeza…asitokee mtu atakaejaribu kuuchelewesha mradi huo, sisi
kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla
hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo muhimu kwa taifa letu.” Alionya.
Alisema mradi huo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni muhimu,
bwawa hilo ni kubwa sana aliwataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji
yanayoelekea kwenye mto Rufiji ili kuwepo uhakika wa upatikanaji wa maji ya
kutosha ni bwawa hili litahitaji maji kwenye ujazo wa mita za ujazo bilioni
33.2 hivyo maji ya kutosha yatahitajika.
"Bwawa hili ni kubwa kati ya mabwawa 70
duniani bwawa la JNHPP ni bwawa mojawapo, kati ya mabwawa manne makubwa Afrika
bwawa hili ni mojawapo na ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki kwa hivyo
Watanzania wanayo kila sababu ya kujivunia na ni wajibu wetu kuyinza na
kuhifadhi vyanzo vuya maji." Alisisitiza.
Alisema
manufaa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa,
kusambaza umeme vijijini na kwenye viwanda, pia utasaidia sana kupunguza
uharibifu wa mazingira.
Awali akitoa
taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa tangu
uzinduliwe na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi
Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)
alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja
namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine
kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande
wa pili kupitia daraja hilo.
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akitoa tathmini yake mbele ya sehemu ya kuingilia kwenye handaki la kuchepusha maji (diversion channel) la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji Mkoani Pwani leo Jumapili Septemba 8, 2019 wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme wa Megawati 2115.
Daraja namba mbili la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika leo Jumapili Septemba 8, 2019.
Kijiko kikitoka kwenye handaki la kuchepusha maji leo Septemba 8, 2019.
Waziri Dkt. Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali kwenye eneo la mradi
Msafara wa magari ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ukipita kwenye daraja namba mbili linalokatisha mto Rufiji leo Septemba 8, 2019.
Waziri Mhe. Dkt. Kalemani (katikati) akipatiwa maelezo na Mratibu wa mradi huo Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara
Ujenzi wa nguzo za daraja namba moja litakalounganisha pande mbili za mto Rufiji ukiwa unaendelea. Daraja hilo litasaidia kuvusha vifaa vya ujenzi (mashine) kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili ili kusaidiana na daraja namba mbili ambalo tayari linafanya kazi.
Eneo la kuingilia ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Dkt. Kalemani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephene Kebwe na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Rufiji (OCD) Lepold Fungu, akipatiwa maelezo na Mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.
Mhe. Dkt. Kalemani akimsikilzia Meneja Mradi kutoka kampuni ya Arab Contractor ya Misri, Mhandisi Mohammad Samaha.(kushoto).
Daraja namba mbili likiwa limekamilika na kufanya kazi
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (JNHPP), ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Steven Manda, mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019.

Post A Comment: