Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akizungumza  na Viongozi wa Wilaya ya Momba wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilaya ya humo.
 Mafundi wakiendelea kuchimba msingi katika ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilayani ambapo ujenzi wa Soko hilo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na kugharimu shillingi bilioni nane.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akikagua mchoro wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilaya ya Momba ambapo kukamilika kwa ujenzi wa Soko hilo kutasiadia wakulima kuuza mazao yao kwa bei nzuri.

MKUU wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameagiza ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilaya ya Momba ufanyike mchana na usiku kutokana na kuchelewa kuanza.
Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo hilo jana jioni alipotembelea eneo la ujenzi wa Mradi huo na kukagua maendeleo ya ujenzi huo ambao mpaka kukamilika kwake utagharimu shilingi shilingi bilioni 8 na mpaka sasa serikali imetoa shilingi bilioni 2.
“Naagiza ujenzi huu ufanyike Mchana na Usiku kwani tuko nyuma ya muda kwa Zaidi ya miezi mitatu, Mkurugenzi hakikisha hilo linafanyika na Tanesco ninawaelekeza waweke umeme hapa ili mafundi hawa wakamilishe kazi hii kwa muda muafaka”, ameelekeza Brig. Jen. Mwangela.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Soko hilo la mazao ni Mkombozi kwa wakulima wa Wilaya ya Momba na Mkoani Songwe kwani watapata sehemu ya kukusanyia mazao ya na kuyauza kwa bei sahihi kuliko kufuatwa na walanguzi mashambani ambao huwapunja.
“ Soko hili litawaokoa wakulima hawana mahali pa kuuzia mazao yao, kuna wao wanaenda huko wanawadanganya na kuchukua mazao yao kwa bei nafuu sana lakini Mkulima wetu akipata nafasi ya kufikisha mazao yake katika soko hili akaja kuyauza mwenyewe atauza kwa bei nzuri”, amesisitiza Brig. Jen. Mwangela
 Aidha amewataka mafundi wanaojenga soko hilo kuonyesha ufundi wao kwa kujenga kwa viwango na kwa kasi nzuri ili wakulima wanufaike na mafundi nao wanufaike kwa kukamilisha ujenzi kwa muda mfupi ili wapate faida.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: