Taasisi ya Utafiti wa  viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) imewataka wakulima kuepuka matumizi ya viuatilifua ambavyo havijasajiliwa na kukaguliwa na taasisi hiyo

Akizungumza hapo Jana katika kongamano la wadau wa kilimo hifadhi lililo andaliwa na shirika la Echo kwa kushirikiana na taasisi ya TPRI na kufanyikia katika ukumbi wa taasisi hiyo mkoani Arusha, mkurugenzi wa huduma za kiufundi TPRI Bw Ephraim Njau amesemakuwa katika kuhakikisha taasisi hiyo inasaidia dhana ya kilimo hifadhi taasisi hiyo imejikita katika kutoa semina za matumizi ya viuatilifu ambavyo haviaribu mazingira, kuhakikisha viuatilifu vinavyotumiwa na wakulima vimekaguliwa, kusajiliwa na taasisi hiyo ikiwemo pia kufanya utafiti wa visumbufu katika mazao

Aidha ameongezakuwa kilimo hifadhi Ni suala muhimu Sana katika kuhakikisha kwamba kizazi Cha leo na kijacho vinakuwepo,wingi wa chakula unakuwepo na malighafi tunazalisha bila kuharibu mazingira

"Kilimo kisipofanywa inavyotakiwa huwa kina madhara kwenye mazingira na katika maisha ya binadamu"alisema Njau
Share To:

msumbanews

Post A Comment: