Saturday, 14 September 2019

TALIRI, TVLA TANGA FRESH KUJA NA MIKAKATI YA SEKTA YA MAZIWA

 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) kituo cha Tanga Dkt. Zabron Nziku akizungumza na waandishi wa habari wa Habari za Kisayansi  kutoka mikoa ya Tanga,Pwani na Morogoro waliotembelea taasisi hiyo 
  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) kituo cha Tanga Dkt. Zabron Nziku akizungumza na waandishi wa habari wa Habari za Kisayansi  kutoka mikoa ya Tanga,Pwani na Morogoro waliotembelea taasisi hiyo huku akiwa ameshika moja ya chakula kizuri ambacho kinatumiwa na mifugo 
  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) kituo cha Tanga Dkt. Zabron Nziku akiwaonyesha  waandishi wa habari wa Habari za Kisayansi  kutoka mikoa ya Tanga,Pwani na Morogoro waliotembelea taasisi hiyo namna wanavyoyapaki malisho ya mifugo na kuyahifadhi tayari kwa ajili ya matumizi 
Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi kulia akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari za sayansi wakati wa ziara hiyo
 Meneja wa Vyanzo vya Maziwa wa Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga Anadomina Nyanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo

WAANDISHI wa Habari za Kisayansi  kutoka mikoa ya Tanga,Pwani na Morogoro wamefanya ziara ya  kutembelea kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresha na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) Wakala wa Maabara za Vetineri (TVLA) 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) kituo cha Tanga Dkt. Zabron Nziku alisema kwamba taasisi hiyo wameandaa mikakati ya kuwawezesha wafugaji waweze kuzalisha maziwa yenye ubora kwa kufanya utafiti wa malisho bora ya mifugo,uzalishaji wa mitamba bora,utafiti wa chanjo bora za mifugo na kutoa mafunzo ya ufugaji wa kibiashara kwa wafugaji.

Alisema kwamba mpango huo ni kuhakikisha sekta ya maziwa nchini hususani mkoani Tanga inakuwa na tija kwa wafugaji na viwanda vya maziwa katika nyanja ya masoko ya ndani na nje ya nchi inakuwa na ushindani kutokana na ubora,

Ziara hiyo imewezeshwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)baada ya kuendesha mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za kisayansi kutoka mikoa hiyo iliyofanyika Jijini Tanga.

 Dkt. Zabron  amesema kuwa taasisi hiyo wanafanya utafiti wa malisho bora ya wanyama na kuzalisha mitamba bora ya ng'ombe na mbuzi na kuwazuia wafugaji.

Amesema kuwa katika upande wa uzalishaji wa mitamba bora ya ng'ombe na mbuzi wanchanganya mbegu za jamii ya aina tofauti za ng'ombe na mbuzi ili kupata aina moja ambao watakuwa na ubora zaidi ambao watakuwa wanatoa maziwa mengi na yenye ubora halafu wanawauzia wafugaji ili kuweza kufuga kibiashara.


Amefafanua kuwa kwa upande wa malisho bora TALIRI wanashirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo ya nchini Kenya(ILRI) kufanya utafiti na majaribio ya malisho bora tofauti ya  mifugo kwa kuchanganya aina tofauti za vinasaba kupata malisho bora.


 " TALIRI kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo(ILRI)ya Kenya tunafanya utafiti wa malisho bora ya mifugo na pia hapa Tanga tunazalisha mitamba bora ya ng'ombe wa maziwa pamoja na mbuzi wa kisasa na kuisambaza kwa wafugaji "alisema.


 Meneja wa  Wakala wa Maabara za Vetinari(TVLA)mkoani Tanga Dkt. Imna Malele amesema kuwa taasisi hiyo katika kuhakikisha afya ya mifugo inakuwa nzuri, TVLA kupitia Taasisi ya Chanjo za  Wanyama(TVI) wamefanya utatiti na kugundua chanjo bora za mifugo ambazo zinaendana na vimelea vya mifugo iliyopo nchini.


Amesema kuwa tangu chanjo hizo zianze kuingizwa sokoni zinaweza kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na mifugo kwa asilimia kubwa na kuongeza ubora wa mazao ya mifugo kutokana zimetengenezwa kwa kuzingatia vimelea vya mifugo iliyopo nchini.


Kuhusu ugonjwa wa Nagana kwa mifugo unaosababishwa na kuenezwa na Mbung'o TVLA wamegundua kemikali ambazo zina harufu inayofanana na mnyama aina ya kuro ambao ni adui kwa Mbung'o.


 Amesema kuwa mnyama(ng'ombe) atafungwa nayo kwenye sikio kwa kutumia kifaa maalum ambapo akijitikisa harufu inaenea na kufukuza Mbung'o.


 Meneja wa Vyanzo vya Maziwa wa Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga Anadomina Nyanga amesema kuwa katika kuhakikisha wafugaji wanaongeza idadi ya uzalishaji wa maziwa wameandaa mkakati mbalimbali ya kumuwezesha mfugaji kufuga kwa tija.


 Amesema kuwa Tanga Fresh kwa kushirikiana na TALIRI na Chama cha Ushirika cha Maziwa cha Tanga(TDCU) wanatoa mafunzo kwa wafugaji katika ufugaji wenye tija na wa kupunguza gharama ili kuinua kiwango cha uzalishaji wa maziwa ili kuiwezesha kiwanda hicho kufikia malengo yake ya uzalishaji wa maziwa na bidhaa za maziwa na tayari wamekwishawafikia wafugaji 3,000.


 Amesema kiwanda hicho kwa siku kinahitaji maziwa lita 120,000 lakini uzalishaji uliopo ni kati ya lita 30,000 na 50,000.


 Ametaja mkakati mwingine ni kuanzisha utaratibu wa kumlipa mfugaji kwa mtindo wa ubora wa bidhaa (quality based payment) ambao amesema utaleta ushindani kwa mfugaji na ilianzia nchini Zimbabwe na kwa Tanzania utakuwa ni wa kwanza
>
> Mwisho

No comments:

Post a Comment