Balaza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) liimetangaza kuongeza muda wa udahili kwa waombaji mafunzo kwa ngazi ya Cheti na Diploma kwa kufungua dirisha dogo la udahili kwa lengo la kuwapa nafasi wale ambao hawakupata nafasi katika udahili wa kwanza au kukosea chaguzi wanazostahili.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt Leonard Akwilapo, amesema wameamua kuongeza mda wa udahili kwa sababu wanatambua kuna idani kubwa ya waombaji hawakupata nafasi na wengine walikosa sifa kwa kozi husika waliyoiomba.

“Wizara imeagiza balaza la taifa la elimu ya ufundi(NACTE) kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia tarehe 7 mpaka tarehe 21 Septemba, 2019,  ili kujaza nafasi zilizo kwenye vyuo na taasisi mbalimbali za mafunzo za serikali na binafsi  katika kada mbalimbali ambazo zina nafasi ya udahili” amesema Dkt Akwilapo.

Aidha amesema Wizara inatoa rai kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita,  na wale wote waliokosa sifa za kujiunga na mafunzo mbalimbalikutumia fulsa hiyo kufanya maombi ya udahili upya, waombaji  wametakiwa  kuwa makini ili wasije kukosa nafasi ya kujiunga na mwaka wa masomo kwa mwaka 2019/2020.

Aidha amebainisha kuwa kwa waombaji wa kozi ya ualimu kwa  ngazi za  cheti na Diploma udahili ulianza tarehe 3 mwezi wa saba hadi tarehe 30 mwezi wa Nane, 2019, waombaji walielekezwa walielekezwa kuomba kupitia tuvuti ya NACTE kwa waombaji wa vyuo vya serikali na vyuo binafsi walielekezwa kuomba moja kwa moja vyuo wanavyotaka.

“Lakini hadi mwisho wa tarehe ya udahili, waomba walikuwa 7,025 waliokamilisha maombi yao, na waliokidhivigezo walikuwa 5,252(75%) na 1,773(25%) hawakuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na mafunzo ya ualimu,  wakati nafasi zilikuwa 12,859 katika vyuo 35 vinavyotoa mafunzo hayo” amesema.

Pia amebainisha jumla ya waombaji 11,028, walichaguliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) na NACTE na kupangiwa vyuo vya mafunzo ya ualimu na majina yao yanapatikana kwenye  tuvuti ya  ya Wizara na NACTE.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha udahili wa NACTE, Twaha Twaha, amewatahadharisha waombaji hasa wa kitengo cha Nessing na Clinical Medicine lazima wawe na ufaulu katika masomo  ya Physics, Chemistry na Biology lazima vizingatiwe katika maombi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: