Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba ametimiza ahadi zake alilzo zitoa jimboni kwake Iramba Magharibi Aprili mwaka huu,ameyasema hayo hivi leo alipokuwa akikabidhi shehena vifaa kwaajili ya umaliziaji wa jingo la zahanati na shule yaliyo ezuliwa na upepo Aprili.

Mwigulu amesema kuwa ameyafanya hayo baada ya ahadi yake na maombi aliyoyapata kutoka kwa wananchi alipofanya ziara Aprili mwaka huu kwenye maeneo hayo kushuhudia madhara ya upopo ulioezua paa la hosipitali.

Baadhi ya vifaa alivyotoa mbunge huyo kwaajili ya zahanati au waliitumia kama kituo cha Afya cha Doromonyi ni pamoja na mbao kwaajili ya kuwekea paa,misumari,rangi,jipsam,mabati na chuma.

Aidha aliongezakuwa pia aliamua kutoa saruji shule ya msingi Mikilango mifuko hamsini kwaajili ya kusaidia kuweka sakafu katika madarasa matatu yaliyokuwa yameharibika.

Aidha pia amewataka wananchi kuacha kuutolea maneno mabaya mradi wa usambazaji umeme vijijini ujulikanao kama REA kwa kusema kuwa wanaweka nguza na kuziacha bila kuweka nyaya bali amewataka kuwa na subira wakati watendaji wa kuu wa mradi huo wakiendelea na usambazaji wa nguzo na nyaya kwa awamu kufuatana na jinsi utaalamu wa uwekaji ulivyo.

Ameongezakuwa serikali ya awamua ya tano ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli imefanya kazikubwa kuhakikisha vijiji zaidi ya elfu saba vinapata umeme ukilinganisha ilivyokuwa awali.

‘’tumuunge mkono rais wetu huwa halali anakesha kuhakikisha wananchi wake mnapata maendeleo kwasasa kwa maendeleo yoote aliyoyafanya  yameshazidi asilimia ya ilani iliyowekwa kwenye ilani ya CCM’’ alisema Nchemba.

Kuhusu miundombinu ya barabara amezidi kumshukuru Rais kwa kuwezeshwa kujengwa kwa barabara katika jimbo lake na kuzipandisha viwango barabara ambazo zilikuwa na hali mbaya na kushindwa kupitika kipindi cha mvua.

Mwigulu anatarajiwa kufanya ziara yake kwa siku kadhaa kwenye jimbo lake akikagua miradi mbalimbali ikiwemo ya Shule,Barabara,Hospitali na mingine ya kijamii na pia kusikiliza kero mbalimbali za wapigakura wa jimbo la Iramba Mgharibi na kuzifanyia utautuzi.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: