Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha Ndugu Omary Bahati Lumato amendelea na Ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya hiyo katika kata ya Moivo ambapo wamefanya Ukaguzi wa madaftari ya wanachama wa Kata hiyo.

Ndugu Omary Lumato , amewataka Vijana kushikamana kwa Pamoja Kama chachu ya ushindi ya kata ya Moivo katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais 2020.

Pia amewasisitizia Vijana , kushiriki kikamilifu kwenye uandikishaji wa daftar la Serikali za mitaa na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi Serikali ya mitaa.

 Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (Uvccm) Mkoa wa Arusha Ndugu Kimji , amewataka Vijana wa Moivo kukamilisha safu za uongozi na kuziba mapengo ya Viongozi mbalimbali ambazo ziko wazi na akatoa siku 3 ili nafasi hizo zizibwe kikamilifu kwani tunaelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,tusiwe na jeshi nusu

Sambamba na hapo Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arumeru Ndg Lalashe Lengitengi amesisitiza pia suala la maadili kwa Umoja wa Vijana  ili wawe mfano kwenye jamii itakayosaidia kuwa mfano kwa Wananchi wanapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa waweze kuwa na ushawishi mkubwa kwa wapiga kura

Kwa upande wake Katibu wa Uvccm Arumeru Ndugu Hussein malipula aliwaasa vijana kupanga mbinu na mikakati ya ushindi wa Serikali za mitaa hasa kwa kujua madhaifu ya wapinzani wao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: