Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amefungua Kongamano la kimataifa la kijiografia, linalojulikana kama (GAT) ambao linalenga kujadili mabadiliko ya tabia nchi na namna jamii inavyoweza kukabiliana na changamoto hizo.
Akifungua mkutano huo unaofanyijka katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) jijini Dar es Salaam, Dkt. Akwilapo amesema jiografia ndiyo maisha kwa kuwa  inaangalia, Kilimo, Afya, Ajira, na maisha ya kila siku.

“Elimu ndiyo  mkombozi wa maisha, jiografia ni afya, Kilimo na maisha ya kila siku hivyo Jamii inavyopambana na mazingira ndivyo inavyochangia katika  Kukuza uchumi wa nchi husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ameeleza kuwa pamoja na majukumu mengine ya Chuo, Chuo pia kinawajibika kufanya tafiti hivyo kupitia Kongamano la GAT wadau wanapata fursa ya pamoja ya kujadili, kuoneshana namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitikeza katika Jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto ktk sekta zote, hivyo hili  ni eneo ambalo wataalamu wanatoa ushauri wanamna ya kukabiliana nalo kupitia mkutano wa namna hii wa GAT” alisema Prof. Mwakalila.

Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo ambaye ni Mhadhiri MwandamiZi wa Chuo Kikuu Nkwawa Dkt. Evaristoo Haule amesema GAT imejikita kufanya kazi na watafiti, na wanataaluma katika masuala ya Jiografia ikiwemo watunzaji wa wanyama, utunzaji wa Maliasili, uchumi wa viwanda na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kongamano hilo la siku tatu ambalo limeanza leo linashirikisha wadau kutoka nchi zaidi ya tano ikiwemo   Afrika Kusini, Ethiopia, Nigeria, Zambia na wenyeji Tanzania.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano,
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE.
16/9/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: