Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana akiendelea na kutoa mafunzo kwa Wataalamu wa Sekta ya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera wa kati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).


Na Rayson Mwaisemba.

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo utaingia nchini.

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo juu ya njia bora yanamna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kuzingatia taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyokatika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga hilo.

Dkt. Sanga amesema kuwa, taarifa za Shirika la AfyaDuniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi yaWagonjwa 2950 wamethibiti kakuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa 2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipo jitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 katiyao wamepoteza maisha.

Aidha,  Sanga amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingi inchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

"Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo  litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu” AlisemaDkt. Alex Sanga.

Hatahivyo, Dkt.  Sanga amesemakuwa, Shirika la AfyaDuniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoahuduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu.

Aliendelea kusisitiza kwa kutoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata mwongozo wa kati wa kutibu ugonjwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: