Tuesday, 17 September 2019

BENKI YA CBA YAANZA KUTOA MIKOPO YA UJENZI


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Benki ya Biashara Afrika (CBA ) imeanza  kutoa mikopo ya ujenzi kwa ajili ya  kuwawezesha wateja wake kuweza kujenga na kumiliki nyumba kwa kupata mkopo rafiki ambao utawawezesha kujenga na kulipa kwa urahisi.

Akizungumza katika siku maalumu ya Wateja wa benki hiyo (customers day) ,Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko amesema kuwa wanatoa mikopo ya ujenzi  kulingana na uwezo wa mteja kulipa mkopo ,pia kulingana na faida anazozipata mteja katika biashara yake ,mkopo huo  umeangalia mahitaji ya wateja wao ya  kumiliki nyumba za ndoto zao.

‘Kwa sasa pia tuna mikopo maalumu kwa Wafanyakazi walioko serikalini ili waweze kunufaika na fursa za mikopo iliyoko katika benki zetu” Anaeleza Mkurugenzi huyo

Anasema kuwa wameanzisha huduma maalumu kwa ajili ya watalii kupata huduma za kifedha kubadilisha fedha za kigeni pamoja na huduma nyingine za kifedha.

Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na wateja binafsi ,Julius Konyani anaeleza juu ya  siku ya leo ambayo wanakutana na wateja wetu tunawashukuru kwa biashara wanayotupatia na kupata mrejesho juu yale ambayo benki yao inafanya.

Julius alisema kuwa Wateja wao wanahitaji makazi ya kudumu walihitaji kuwa na viwanja na kuanza ujenzi ,tunawakopesha mkopo wa kununua viwanja na kujenga wanaulipa kwa miaka 20.

No comments:

Post a Comment