Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega pamoja na wananchi wa Jimbo la Mkuranga wakichangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Bi. Wema Msafiri akiwashauri wananchi wa Jimbo la Mkuranga kabla ya kuanza shughuli ya kuchangia damu.
Wananchi wa Jimbo la Mkuranga wakisikiliza maelekezo kabla ya kuchangia damu leo.
Mmoja wa wakazi wa Mkuranga akichukuliwa vipimo na mtaalam wa MNH.
Baadhi ya vijana wakiwa katika foleni ya kufanya vipimo mbalimbali kabla ya kuchangia damu hospitalini hapa.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wakazi wa Mkuranga katika eneo la MNH.
Vijana wakisubiri kufanyiwa vipimo kabla ya kuchangia damu leo.



Na John Stephen

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega pamoja na wananchi wa Jimbo la Mkuranga wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuchangia damu kwa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro Jumamosi iliyopita.

Akizungumza wakati akichangia damu, Mhe. Ulega amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa kuwa kiasi kikubwa cha damu kinahitajika kwa majeruhi hao pamoja na wagonjwa wengine wenye uhitaji.

Mhe. Ulega ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga amesema kuwa amefika MNH pamoja na zaidi ya wananchi 50 kwa ajili ya kuchangia damu majeruhi hao ambao wamelazwa katika wodi mbalimbali.

“Tupo hapa kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi waliopata ajali ya moto, lakini pia tunamuunga mkono Rais wetu aliyekuwa wa kwanza kufika hapa Muhimbili lakini pia alimuagiza Waziri Mkuu, mh. Kassim Majaliwa kushiriki msiba kwa siku tatu mfufulizo, hivyo sisi hatuna namna zaidi ya kuunga mkono jitihada za viongozi wetu,” amesema Mhe. Ulega.

Mhe. Ulega amewataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangia damu kwa kuwa hospitali nyingi nchini zina upungufu wa damu hivyo watu wajitokeze ili kuokoa maisha ya majeruhi wanaopata ajali .

Juzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Magufuli alitembelea majeruhi wa ajali ya moto waliolazwa MNH na kuahidi kulipa gharama zote za matibabu, dawa na chakula kwa majeruhi wote.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: