Wednesday, 28 August 2019

UPDATES: Viongozi wa maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege Ya Tanzania Inayoshikiliwa Afrika Kusini wakamatwa na Jeshi la Polisi

Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi walioanzisha maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini wamekamatwa  na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  Lazaro Mambosasa, amesema jeshi la polisi  limeyatawanya maandamano hayo kwa kuwa hayana kibali.

Mambosasa amewataka watanzania wawe watulivu kwa kuwa serikali imeshaanza kulishughulikia suala hilo la ndege ya Tanzania  inayoshikiliwa Afrika Kusini

No comments:

Post a Comment