Friday, 30 August 2019

MEYA WA ILALA AGIZA IDARA YA UHANDISI ILALA KWENDA NA KASI YA RAISNA HERI SHAABAN(BUYUNI)

MEYA wa Halmashauri ya Ilala Omry Kumbilamoto ameitaka Idara ya Uhandisi halmashauri ya Ilala kufanya kazi kwa kasi ya Rais John Magufuli bila kukwepa majukumu ya idara hiyo.

Meya KumbiIamoto haliyasema hayo Kata ya Buyuni wilayani Ilala leo wakati alipokwenda kufufua greda la halmashauri hiyo ambalo liliegeshwa mtaa wa Nyeburu kwa kukosa betri hali iliyopelekea kero kwa wananchi   katika mitaa yenye barabara mbovu.

"Nakuagiza mhandisi wa Halmashauri ya Ilala changamoto zingine katika idara yako tatua mwenyewe usimsubiri Meya ili afike au Mkurugenzi wa Ilala kwani kufanya hivyo inaleta kero kwa kukwamisha kazi za halmashauri"alisema Kumbilamoto.

Aliagiza idara hiyo kubadika kufanya kazi kwa weledi inapotokea tatizo  kulitolea taarifa kwa wakati ili kama kuna changamoto zitatuliwe uwezi kulaza greda kwa muda mrefu wanachi wanapiga kelele barabara mbovu zinashindwa kukarabatiwa kwa wakati kwa kigezo cha Kukosekana betri sawa na kurudisha nyuma juhudi za utekelezaji w llani ya Chama cha Mapinduzi.

 Meya wa Ilala aligharamia mabetri  yenye thamani ya shilingi 900,000/= greda hiĺo  fedha iliyotolewa na wadau wa Maendeleo wa wilaya hiyo.

Aliagiza greda hilo zitatuwe changamoto za jimbo la Ukonga zote baada hapo ligamie wilaya nyingine.

Aliagiza dereva achonge barabara zote za Buyuni  alafu lihamie Pugu na Ulongoni baada hapo ratiba zingine ziendelee.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyeburu Hamisi Gea alimpongeza Meya Ilala kwa kutatua tatizo hilo  .

Mwenyekiti Gea alisema kwa sasa katika halmashauri ya Ilala wamepata meya mchapa kazi ambaye anatatua kero kwa wakati na kutekeleza Ilani kwa vitendo kwa kusaidia wanyonge.

Mwisho
Agosti 29/2019
Kata ya Buyuni

No comments:

Post a comment