Saturday, 10 August 2019

Diwani Mwingine wa CHADEMA Arumeru Atimkia CCM

Diwani wa kata ya UsaRiver  wilayani Arumeru Mkoani Arusha kuptia chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) Ndugu Henry Mpinga amejiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi  CCM.

Akizungumza leo August 10 Mpinga amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, John Magufuli na Juhudi kubwa za kuwaletea wana Arumeru maendeleo zinazofanywa na mbunge wa Jimbo hilo la Arumeru Mashariki Dr. John D Pallangyo .