Serikali ya Wanafunzi ya Chuo kikuu Mzumbe imekutana na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa lengo la Kubadilishana uzoefu  katika matumizi ya kadi za bima ya Afya kwa wanafunzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washauri wa Wanafunzi wa vyuo hivyo akiwemo Ukende Mkumbo wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere amesema kadi ya bima ya Afya kwa wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho ni lazima ili kuepusha usumbufu mwanafunzi anapougua.
“Kwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kila mwanafunzi lazima akate kadi ya bima ya afya, na ailipie ili iwe active kwa matumizi,”alisema Ukende.
Kwa upande wake Mariam Matao ambaye ni mshauri wa Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe amesema kadi hizo ni mkombozi kwa wanafunzi huku akiwataka kuzitumia kwa kufuata taratibu na miongozo iliyopo na siyo kuzitumia vinginevyo.

Ziara hiyo ya kikazi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu  Mzumbe pia imetembelea na kuona  namna Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inavyotumia umeme wa jua ( solar power)  chuoni hapo katika mabweni mbalimbali yanayotumiwa na Wanafunzi.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
29/8/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: