Na Ferdinand Shayo,Iringa .
Wakulima wa
nyanya mkoani Iringa wamesambaziwa mbegu
bora za nyanya aina ya Firenze F1 ambazo ni mkombozi wa mkulima zinatoa mazao
mengi na kuhimili magonjwa ya nyanya ambayo yamekua yakiwasumbua wakulima wengi
kupata hasara na kushindwa kunufaika na kilimo.
Mwakilishi
wa kampuni ya Bayer Crop Science zamani ikijulikana kama Monsanto, William
Macha, amesema kuwa nyanya hiyo inaweza kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika
baada ya kuvunwa na kusafirishwa katika masoko ya ndani na nje ili kuwafikia
walaji ikiwa kwenye hali nzuri.
“Mbegu hizi za Firenze FD1 Nyanya “Dum Dum” ukiwa na gramu
25 inatosha kwa ekari moja kwasababu inaota kwa asilimia 99% ,kutoka mche mmoja kwenda mwingine tuweke 45
cm ili uweze kupata mazao ya kutosha na kuvuna kwa awamu mara 8 mpaka 12”
Anasema kuwa
mbegu hizo zinazaa mara tatu zaidi ya mbegu za kawaida na pia inakomaa ndani ya siku 75 na inaweza
kuongeza pato la mkulima na kuboresha maisha yake.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wakulima wa nyanya na mboga mboga Mtokambali Mrisho amesema kuwa
kwa mara ya kwanza mbegu ya Firenze F1 kuingia, ilifanyiwa majaribio katika
kijiji cha Tanangozi Iringa na kufanya vizuri sana baada ya hapo ilipendekezwa
kuwa mbegu bora zaidi na wakulima walianza kuitumia na kupata matokea makubwa.
Mtokambali
amesema kuwa kwa sasa wakulima kutoka mikoa ya Dodoma na Morogoro wanafika
kujifunza kwenye shamba darasa la mbegu hizo ambazo zimeleta mavuno pesa kwa wakulima wengi mko wa
Iringa na viunga .
Post A Comment: